Thursday, February 9, 2012

HABARI KUTOKA MUSOMA


MUSOMA

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KAMUNYONGE MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARAWAMEOMBA KUKUTANA NA MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN TUPA KUFUATIA KUKWAMA KWA UBORESHAJI WA SOKO HILO IKIWA NI NJIA YA KUTAKA KUMUELEZA KERO ZAO.

WAKIZUNGUMZA NA KITUO HIKI KWA NYAKATI TOFAUTI KWA SHARTI LA KUTOTAJWA MAJINA YAO WAFANYABIASHARA HAO WAMESEMA KUWA KUMEKUWA NA KAULI KINZANI KWA BAADHI YA VIONGOZI WA HALMSHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA KITU AMBACHO KINASABABISHA KUDHOROTA KWA UTEKELEZAJI WA SOKO HILO.

WAMESEMA WAMECHOKA NA AHADI ZISIZOTEKELEZEKA ZA VIONGOZI WA MANISPAA AMBAZO ZINAONEKANA KUWA ZINASUKUMWA NA SIASA BADALA YA KUTEKELEZA SOKO HILO.

WAKITOA UFAFANUZI BAADHI YA KERO ZINAZOWAKABIRI KATIKA SOKO HILO, WAFANYABIASHARA HAO WAMESEMA KUWA NI PAMOJA NA KUTOKUWEPO KWA MAPIPA YA TAKA KITU AMBACHO KINASABABISHA UCHAFUZI WA MAZINGIRA.

KUFUATIA KERO NA MALALAMIKO HAYO WAFANYABIASHARA HAO  WAMEMUOMBA MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN TUPA KUINGILIA KATI SUALA HILO NA KULIPATIA UFUMBUZI IKIWA NI NJIA YA KUWAJENGA MAZINGIRA MAZURI YA BIASHARA HIYO

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA  DK. KALAINE KUNEI AMESEMA KUWA SUALA LA UCHELEWESHWAJI WA MAHINDI YA CHAKULA CHA MSAADA NI LA KITAIFA NA SI MZABUNI ALIEPEWA TENDA YA KUSAMBAZA MAHINDI HAYO.

HAYO AMEYASEMA JANA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBU WA MIKUTANO WA HALMASHAURI HIYO MJINI MUSOMA MKOANI MARA

AMESEMA KUMEKUWA NA UPUNGUFU KATIKA GHALA LA TAIFA LA CHAKULA MKOANI SHINYANGA KUTOKANA NA KUHUDUMIA MIKOA YA KANDA YA ZIWA HALI ILIYOPELEKEA KUWEPO NA FOLENI YA MAGARI MKOANI HUMO INAYOSUBIRI KUPAKIA MAHINDI HAYO.

DR. KUNEI AMESEMA KUWA BAADHI YA KATA KATIKA HALMASHAURI HIYO YA MUSOMA ZIMEKWISHA PATA MAHINDI HAYO NA AMBAZO BADO HAZIJAPATA ZINAENDELEA KUSHUGHULIKIWA

AWALI DIWANI WA KATA YA NYAMIMANGE NYASWE CHACHA ALIHOJI KITENDO CHA BAADHI YA KATA KUPEWA MGAWO WA MAHINDI MARA MBILI WAKATI KATA NYINGINE ZIKIWA BADO HAZIJAPATA HALI ILIYOPELEKEA BAADHI YA MADIWANI WENGINE KULIZUNGUMZIA SUALA HILO.

AKIZUNGUMZIA SUALA LA ELIMU KATIBU TAWALA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA BI. DEBORA MAKINGA AMEOMBA MADIWANI WA HALMASHAURI HIYO KUSIMAMIA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA VILIVYOBAKI ILI KILA MWANAFUNZI ALIEFAULU KWENDA SEKONDARI AWEZE KUPATA NAFASI HIYO.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment