Sunday, July 13, 2014

Wananchi Butiama waua Majambazi 3 kwa kuwachoma moto


 WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuwawa kwa kushambuliwa na siraha za jadi ikiwemo rungu,mapanga na mawe baada ya kudaiwa kufanya uhalifu wa kuwateka wavuvi ndani ya ziwa Victoria na kuwanyang’anya vifaa vyao vya uvuvi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mara Philip Karangi alisema tukio hilo lilitokea julai 9 majira ya saa 5 usiku katika kisiwa cha Iriga kilichopo Kijiji cha Busamba Kata ya Etaro Wilaya ya Butiama.

Wednesday, July 2, 2014

POLISI TABORA YANASA MAJAMBAZI WATANO NA BUNDUKI MOJA ,JAMBAZI MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari silaha aina ya SMG iliyokamatwa ikiwa na risasi mbili pamoja na watuhumiwa watano ambapo mmoja kati ya watuhumiwa hao aliyefahamika kwa jina moja la Rajab anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-36 alifariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi huko katika kijiji cha Tura wilayani Uyui. Aidha majambazi hayo yalikamatwa baada ya kufanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha ambapo yalifanikiwa kupora zaidi ya shilingi milioni mbili na laki tatu na ndipo makachero wa Jeshi la Polisi kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi walifanikiwa kuyakamata yakiwa na silaha hiyo ambayo imedaiwa ilitumika katika tukio la uporaji pamoja na Pikipiki mbili aina ya Sanlg
Kamanda Suzan akionesha magunia  mawili na nusu ya bhangi yaliyopatikana katika msako mkali wa Jeshi la Polisi huko eneo la Wilaya ya Nzega ambapo watu watatu wanashikiliwa kuhusiana na tukio la kuwa wauzaji na watumiaji wa bhangi.


Tuesday, July 1, 2014

Biashara United Musoma yaibamiza Polisi Veteran Musoma mabao 2-0Na Mwandishi wetu

Timu ya soka ya Biashara United ya mjini Musoma Mkoani Mara inayojiandaa ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwishoni mwa wiki imewabamizia Timu ya Polisi Veteran ya Mjini Musoma mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini hapa.


Mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina ya ufundi kutoka kwa wachezaji wa timu zote kipindi cha kwanza kilimalizika baada ya timu hizo kutosha nguvu ya 0-0 

Katika kipindi cha Pili timu hiyo inayoongozwa na Kocha Mchezaji Aman Richard ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ambapo katika safu ya ushambuliaji aliingia Augustine Mgendi mabadiliko ambayo yaliinufaisha timu hiyo ya Biashara United baada ya mchezaji huyo kuifungia timu hiyo mabao hayo mawili.

Akiongea baada ya mchezo huo,Kocha huyo alisema kuwa bado timu hiyo inahitaji kufanya maboresho kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge Mjini Dodoma.

Tumeshinda mchezo wetu lakini bado tuna kazi kubwa maana tunapata nafasi nyingi lakini hatuzitumii ipasavyo,sasa kwa mchezo uliopo mbele yetu lazima tubadilike” alisema Kocha Aman

Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani hapa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi August mjini Dodoma.

Saturday, June 28, 2014

Afande Steven John zamani akifahamika kwa jina la Bebeto alivyomeremeta na wife wake jijini Dar

Ndugu wa Maharusi watarajiwa wakiwa katika ukumbi wa Rombo Green View kushuhudia Send Off ya Mebo Malakasuka
Bw Harusi mtarajiwa Afande Peter Steven John akiwa karibu na rafiki zake wakati wa Send Off  ya mkewe mtarajiwa Mebo Malakasuka.
Bi Harusi mtarajiwa Mebo Malakasuka (shoto)akitabasamu kwa mbaaali wakati wa sherehe ya kumuaga(Send Off)iliyofanyika katika ukumbi wa Green View jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Polisi Morogoro na timu ya Taifa,Thobias John akito pongezi kwa shemeji yake wakati wa Send off iliyofanyika katika ukumbi wa Rombo Green View.
Bw Harusi mtarajiwa akiwaaga ndugu zake mara baada ya kumalizika kwa sherehe ya Send Off ya mkewe mtarajiwa Mebo Malakasuka.
Maharusi wakifurahia kuanza kwa historia mpya katika maisha yao.
Ndugu wa karibu wa Bw Harusi Peter Steven John wakiwa katika picha ya pamoja.
Bi Harusi mtarajiwa akasindikizwa kwenda kupumzika.                                                       

Thursday, June 26, 2014

Waandishi wa Kigoma ndani ya hifadhi za Taifa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro


Mtuhumiwa Tarime afariki mikononi mwa PolisiMaandamano ya wananchi wa mji mdogo wa sirari wilaya ya Tarime mkoani Mara  waliotaka kujua chanzo cha mauaji ya kijana mmoja mkazi wa eneo hilo ambaye anadaiwa kukamatwa na Jeshi la polisi na kisha mwili wake kukutwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime yamesababisha vurugu kubwa na kusimama kwa shughuli mbalimbali za kijamii kwa saa kadhaa
 
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la kitandika Ryoba anadaiwa kukamatwa siku nne zilizopita na askari wa jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kwa tuhuma za kukutwa akicheza kamali  lakini tangu siku ya tukio hilo kijana huyo hakupatikana hadi taarifa za kifo zilipowafikia ndugu zake  na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha Maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime
 
Taarifa hizo zilisababisha  wananchi  wa eneo hilo kufanya Maandamano  ikiwa ni njia ya kushinikiza  jeshi la Polisi kueleza chanzo cha kifo  cha kijana huyo ambapo jeshi la polisi liliingia kati kuzima maandamnao hayo hali ambayo  ilisababisha wananchi hao kuifunga barabara kuu ya inayotumika kwa safari za Mwanza,Tarime na nchi jirani ya Kenya  kwa kutumia Mawe lakini pia wakichoma matairi ya Magari.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Tarime Rorya Kamishana msaidizi Mwandamizi Justus Kamgisha amesema Mtuhumiwa huyo kitandika Ryoba baada ya kukamatwa alifikisha kituo cha Polisi kuhojiwa na wakati Mahojiano yakiendelea alidai kujisikia vibaya ambapo nalikimbizwa hospital na wakati anapatiwa matibau akafariki dunia.