Saturday, April 9, 2016

RC MULONGO atoa wiki mbili kwa Mkurugenzi H/Rorya kuhakikisha Kituo cha Afya Kinesi kinaanza kazi

                           Jengo la kituo cha Afya kinesi kwa nyuma
                           Baadhi ya wananchi wa kinesi wakiwa katika jengo la upasuaji la kituo cha Afya
                          Wananchi wakiendelea kumsikiliza RC Mulongo
                              Vifaa vilivyopo katika kituo hicho

Mkuu wa mkoa wa Mara Bw MAGESA MULONGO ametoa wiki mbili kwa 
Mkurugenzi wa halmshauria ya wilaya ya Rorya kuhakikisha kituo cha Afya cha Kinesi kinaanza kazi ya upasuaji.

Kauli ya mkuu huyo wa mkoa inafuatia kususua kuanza kutumika kwa jengo hilo kutokana na tatizo la kutokuwepo kwa huduma ya umeme na Maji hivyo kusababisha wananchi katika kijiji hicho kutafuta huduma za upasuaji katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Mara.

  " Mkurugenzi na mhe Makamu Mwenyekiti ndani ya wiki mbili nataka kituo hiki kiwe kimeanza kazi,mtajua mtakapotoa hela lakini ninachotaka ni hiki kituo kianze kazi ndani ya siku kumi na nne"alisema Bw Mulongo 

No comments:

Post a Comment