MAITI NYINGINE ZAIDI ZA MV SKAGIT ZAIOBUKA
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Idadi
ya maiti za ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Skagit zimeongezeka na
kufikia 89 baada ya miili mingine 11 kupatikana leo katika maeneo manne
tofauti ya visiwa vidogovidogo vilivypo mwambao wa Zanzibar.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema
kuwa miili iliyopatikana leo, sita ni wanaume akiwemo kijana mdogo na
mingine mitatu ya wanawake.
Inspekta
Mhina amesema, maiti zote zimezikwa katika makaburi ya pamoja ya Kama
yaliyopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar chini ya usimamizi wa Jeshi la la
Wananchi wa Tanzanaia JWTZ, Jeshi la Polisi, MKMK, JKU na Varantia.
Amesema
miili hiyo ilipatikana katika viisiwa vya Pungume, Fumba, Chumbe na
eneo linalokupwa na kujaa maji la Funguyasini maeneo jirani na kisiwa
mama cha Unguja.
Naye
Mkuu wa Polisi Kikosi cha Wanamaji na Bandari Zanzibar SP Martin Lisu,
amesema kuwa kunauwezekano mkubwa kuwa maiti hizo zinaibuka kutoka
katika meli hiyo ya Skagit.
Kamanda
Lisu, amesema kuwa kutokana na kuendelea kuibuka kwa maiti hizo,
Maafisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaendelea na zoezi lao la
kutafuta miili mingine na kupokea taarifa za kuonekana kwa mwili kutoka
kwa watu wenye vyombo binafsi vya uvuvi na kuzifuatilia.
Hivi
karibuni akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Kikwete, Daktari Mkuu Mwelekezi wa Jeshi la Polisi nchini Dk. Ahamed
Makata, alisema kuwa maiti nyungi zitaweza kupatikana ifikapo siku ya
nne tangu kuzama kwa meli hiyo.
Alisema
tabia ya maiti ya binadamu aliyekufa maji na kuzama, haiwezi kukaa
chini ya maji kwa muda mrefu kama haikufungwa na kitu kizito kabla ya
kuzama.
"Kwa
kawaida maiti ya mtu aliyekufa maji haiwezi kukaa ndani ya maji wakati
wote na kwamba hata kama itaendelea kubaki majini lakini katika muda wa
kuanzia siku tatu na nne mwili ama miili hiyo nilazima ianze kuibuka na
kuelea juu ya maji". Alisema Dk. Makata.
Mwisho
MELI YA KALAMA YAPIGWA STOP
Na Mohammed Mhina, wa Jeshio la Polisi zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeipiga marufuku meli ya MV Kalama ambayo ni
pacha na meli ya Skagit iliyozama baharini wiki iliyopita.
Uwamuzi
huo umetangazwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi, wakati akipokea misaada ya fedha kutoka Mfuko wa Pensheni wa
watumishi wa Serikali za Mitaa na Radio Coconut.
Balozi
Iddi amesema kuwa pamoja na kuisimamisha meli hiyo kutoa huduma za
usafiri kwenye bahari ya Hindi, pia imewataka watu wote wanaotaka
kununua meli kuleta kwanza aina na muundo wa meli wanayotaka kuinunua na
imetumika kwa muda gani.
Lakini
amesema meli ambazo zimeshaingia na kusajiliwa, nazo zinafanyiwa
uchunguzi ili kubaini ubora na umri wake tangu ianze kufanya kazi kabla
ya kuingizwa nchini kwa biashara ya kusafirisha abiria.
Hata
hivyo amesema kuwa Serikali inajipanga kununua meli ya uhakika
itakayotoa huduma ya usafiri majini kati ya Zanzibar na Pemba na
Zanzibar na dar es Salaam ili kupunguza mashaka kwa wasafiri.
Mfuko
wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali za Mitaa NLPF kupitia Mkurugenzi
wake Bw. Andrew Kuyeyama umetoa shilingi milioni 5 na Bw. Ali Khatibu
Dai wa Radio Coconut ametoa mchango wa shilingi milioni moja zote zikiwa
kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu na za mazishi kwa wafiwa.
No comments:
Post a Comment