Wadau wakitaza picha walizopiga
Mwakilishi wa Vfm Mara akifanya mahojiano na mkuu wa wilaya ya Serengeti juu ya kifo cha Mwl James Irenge
Ndege iliyombeba Waziri mkuu Pinda ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Musoma leo Asubuhi
Waziri mkuu akisalimiana na Viongozi baada ya kufika katika uwanja wa Ndege Musoma
Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za Mwisho kwenye Jeneza la hayati Mwl James Irenge leo mjini Musoma
Mke wa Waziri mkuu Tunu Pinda akitoa heshima za Mwisho
Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mh Vincent Nyerere akitoa heshima za Mwisho kwenye Jeneza la hayati mwalimu James Irenge
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mh Nimrodi Mkono akitoa heshima za Mwisho kwa Hayati Mwalimu James IrengeAliyewahi kuwa mbinge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo akitoa heshima kwenye jeneza la hayati Mwl James Irenge
Musoma'
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameongoza Mamia ya Wananchi mkoani Mara kumuaga aliyekuwa Mwalimu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage,Mzee James Irenge katika kijiji cha Busegwe wilayani Butiama mkoani Mara
Akitoa salaam za rambirambi nyumbani kwa Marehemu James Irenge Musoma mkoani Mara,Waziri mkuu Pinda amesema kuwa Mzee Irenge mbali na kutofahamika sana lakini alikuwa ni mtu mwenye historia kubwa nchini kutokana na Mchnago wake wa kumlea Nyumbani kwake na kumfundisha darasani Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika shule ya Mwisenge mjini Musoma darasa la tatu na nne
Akisoma maombi maalum ya Familia ya Marehemu mzee James Irenge kwa Waziri mkuu,mmoja wa wanafamilia Bw Arthur Irenge amemuomba waziri mkuu kusaidia Familia hiyo kupata kiinua Mgongo alichostahili kulipwa baada ya kustaafu kazi mwaka 1970.
No comments:
Post a Comment