Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa akisoma taarifa ya serikali
Mkuu wa Mkoa akisalimiana na Baadhi ya wageni katika Maadhimisho hayo
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara Kamishina Mwandamizi wa jeshi la Polisi Abslom Mwakyoma
Mkuu wa mkoa wa Mara akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani Mara
Furaha pale watu wanapokutana na kukumbushana mambo ya nyuma
Mnara uliowekwa katika eneo ambalo ndege ilianguka

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa mkoani Mara
yamefanyika leo katika Viwanja vya Kanisa
la RC Rwamlimi huku mgeni rasmi akiwa mkuu wa mkoa wa Mara Bw. John Tuppa.
Katika Madhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa
amesema kuwa ipo changamoto kubwa kwa viongozi wa Manispaa ya musoma,wadau
na viongozi mbalimbali kuwaenzi Mashujaa waliosaidia kuikomboa nchi Tanzania.
Amesema ni vyema wananchi wa mkoa wa Mara kuendelea
kufuata nyayo za Mashujaa wetu,kulinda hazina za Ujasiri,Uzalendo,Umoja na
Mshikamamo walizotuachia.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mara amesema kuwa watanzania
wasiichee Amani tuliyonayo kwani haikujengwa siku moja na kama tutathubutu
kuiacha itaondoka Mara moja lakini itatugharimu muda mwingi na jasho jingi
kuirudisha.
Amesema ni vyema wananchi wakashiriki vizuri katika Zoezi la Sensa litakaloanza
August 26,2012 na pia kuhudhuria kwa wingi ili kutoa maoni yao kwa furaha na
Amani pale tume ya kupokea maoni juu ya katiba mpya itakapopita kwenye maeneo
huska.
Mkuu wa mkoa Tuppa amesema maadhimisho hayo
yataendelea kuboreshwa kwa miaka inayokuja ikiwa ni njia sahihi ya kuwaenzi
Mashujaa walioikomboa Tanzania
No comments:
Post a Comment