Saturday, September 1, 2012

Tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya mji wa Musoma 

 Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
 Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
 Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
 Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
 Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
 Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali
Picha na Mtaa kwa mtaa Blog

No comments:

Post a Comment