Saturday, September 1, 2012

POLISI WAUWA WAWILI NA KUJERUHI MMOJA MGODI WA NOTH MARA.

Dinna Maningo,Tarime.

WATU wawili wamekufa na mwingine kujeruhiwa na askari polisi wanaolinda Mgodi wa Dhahabu wa North Mara Nyamongo baada ya kudaiwa kuhusika na kuingia ndani ya mgodi kwa nia ya kupora mawe yenye dhahabu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  ambapo alisema kuwa  watu wanaokadiriwa kuwa 800 maarufu kama intruda wakiwa na silaha za jadi aina ya panga,Nyundo na Mawe walivamia maeneo hayo kwa nia ya kupora dhahabu


Kamugisha alisema kuwa mnamo agost 30 majira ya saa 12 jioni maeneo ya Rompad na shimo la Gokona  wakati polisi wakiwa kwenye jitihada za kuwazuia na kuwaondoa intruda hao  watu wawili waliuwawa baada ya kupigwa risasi na polisi  ambapo Paulo Sarya (26) mkazi wa Nyangoto na Rodgers Mwita mkazi wa Kimusi waliuwawa huku  Mseti Chacha  akijeruhiwa  kwa kupigwa risasi kwenye goti la mguu wa kulia na kulazwa hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Kamugisha alisema kuwa  askari mmoja   No. E 6059 D/CPL Julius amejeruhiwa na maintuda kwa kukatwa panga usoni na kupata majeraha mdomoni na mgongoni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime Marco Nega alithibitisha kupokea mihili ya marehemu wawili  pamoja na majeruhi mmoja anae endelea kupata matibabu hospitali ya Wilaya ambapo kwa upande wa Askari polisi alisema kuwa hawana taarifa yoyote kuhusu askari polisi na hospitali yake haijampokea askari yeyote.

“ Jana  mida ya saa 2 usiku tumepokea mihili ya marehemu wawili Lucas mwita Marwa (20) mkazi wa Kimusi tumemfanyia uchunguzi alipigwa risasi karibu na shingo na kutokezea kifuani upande wa kulia na kuharibu ubavu na mishipa kukatika na kusababisha kuvuja kwa damu nyingi na kusababisha kufa” alisema Nega.

Aliongeza” Mwingine ni Paulo Sarya (26) mkazi wa kijiji cha Matongo alipigwa risasi mguu wa kulia karibu na goti na kutokezea kwenye paja  na kusababisha kukatika kwa mshipa wa damu na hivyo kuvuja damu nyingi na kusababisha kifo,Chacha Mseti(20) mkazi wa Nyamwaga amejeruhiwa  kwa kupigwa risasi mguu wa kulia na yuko wodini anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri hao ndio watu tuliopokea wote wamepigwa kwa risasi za moto nimekagua wodi zote hakuna Askari polisi yeyote aliyepokelewa”alisema Nega.

Hata hivyo Majeruhi Chacha Mseti aliliambia mwananchi wodini hapo  kuwa akiwa barabarani jirani na Mgodi wa Gokona askari wakiwa wanawatawanya watu kwa risasi wanaodaiwa kuvamia mgodi aliweza kushambuliwa na kisha kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

No comments:

Post a Comment