Wednesday, April 23, 2014

Idadi ya waliokufa katika Ajali ya Basi la Luhuye yaongezeka

Dr. Derick David.
IDADI ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya basi la kampuni ya Luhuye lililo pata ajali jana atika eneo la Masanza Kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu majira ya asubuhi likitokea Sirari Mkoani Mara Kwenda Kahama inatajwa kuongezeka kutoka ile ya awali 11 na sasa kufikia 16.

Kwa mujibu wa Dr. Derick David ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dharura Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza amesema kuwa jana idara yake ilipokea watu 35, kati yao watu wawili walifariki dunia wakati wakipewa matibabu, miili ya watu wengine wawili waliletwa ikiwa tayari imepoteza uhai wakati wa harakati za kufikishwa hospitali hapo na mmoja ameongezeka leo akiwa kwenye matibabu hivyo kufanya ongezeko la watu watano na kufikisha idadi ya watu 16 hadi sasa. Source Gsengo




Huku wakisimulia kilichotokea na hatimaye kusababisha ajali hiyo, nao majeruhi walio katika Hospitali ya Bugando wamezugumza.
Huku akieleza kuwa hajui amefikaje katika Hospitali ya Bugando majeruhi ajali ya basi Yohana Peter Milinde anasimulia hatua za mwisho anazo zikumbuka kuhusu mkasa wa ajali hiyo

Ongezeko la majeruhi hospitalini hapo limesababisha msongamano kiasi cha kusababisha wagonjwa kulazwa wawili wawili kwenye vitanda.

Majeruhi wa ajali ya basi Peter Funga naye amelaumu vitendo vya baadhi ya madereva kutozingatia kanuni na sheria zinazowaongoza barabarani hata kusababisha ajali.


No comments:

Post a Comment