Sunday, December 1, 2013

Wajasiriamali nchini watakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora

MUSOMA
 
Shirika la Viwango nchini  TBS limewataka Wajasiriamali  nchini kuhakikishia bidhaa zao zinakuwa na ubora unaostahili ili kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
 
Afisa uhusiano wa Shirika hilo Bi Roida Andusamile alisema Wajasiriamali wengi nchini wamekuwa wakikosa Soko la uhakika la ndani na nje kutokana na bidhaa zao kutokuwa ubora kuanzia wanapozalishia bidhaa hizo.
 
"Ili kupata alama ya ubora kuna vitu vya kuangalia ikiwemo hata eneo la kuzalishia bidhaa huska hivyo basi ni changamoto kwa wajasiriamali kuhakikisha wanazalisha bidhaa zao katika hali ya ubora"alisema  Andusamile 
 
 
Amesema  ili kupata alama ya ubora wajasiriamali hao utambulisho na shirika la viwanda vidogo Sido na kusema kuwa katika shirika hilo la viwango hakuna urasimu kama inavyodhaniwa na kuongeza kuwa liko  mbele katika kutoa elimu kwa Wajasiriamali hao.
 
Baadhi ya wajasiriamali ambao wanashiriki katika Maonyesho hayo ya Kanda ya Ziwa ya Viwanda vidogo yaliyoandaliwa na shirika linaloratibu viwanda hivyo Sido kwa Mwaka 2013 waliothibitishwa na TBS walieleza faida walizopata baada ya kuthibitishwa.
 
  " Kwa kweli tbs imetusaidia sana maana kwa sasa bidhaa zetu tunauza hata nje ya nchi na pia kwenye Supermarket mbalimba hapa nchini"
 


Kufua hatua hiyo Wajasiriammali hao waliwataka wenzao kuhakikisha wanapata alama ya tbs kwani itasaia kuinua kipato chao lakini pia kuboresha bidhaa zao
 
 Maonyesho ya Kanda ya Ziwa ya Viwanda vidogo Sido yaliyoanza Novemba 27 mwaka huu yataitimishwa Desemba 2 katika 

No comments:

Post a Comment