Sunday, December 1, 2013

Vyombo vya habari vyaombwa kuelimisha juu ya HIV

Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo akifungua Semina kwa waandishi wa habari juu ya ugonjwa wa ukimwi


VYOMBO vya habari nchini,vimeombwa kusaidia Taifa katika vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na unyanyapaa,kwani hivi sasa kumebainika kuanza maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi.

Meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo,ametoa  wito huo ,wakati akifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari,juu ya ugonjwa wa ukimwi na kupinga unyanyapaa.


Katika semina hiyo,iliyoandaliwa na Taswa Arusha ,chama cha wanaoishi navvu mkoa wa Arusha(TUPO) na kampuni ya Ms unique na kudhaminiwa na shirikala PSI,Mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF,PSPF,NSSF,LAPF na Shirika la Pingos Forums meya Lyimo,amesema hali ya maambukizi ya vvu ni mbaya.


Amesema  kwa hali ilivyo sasa,ni muhimu vyombo vya habari,kushiriki ipasavyo katika vita dhidi ya Ukimwi kwani hali sio nzuri.


Na kuwa  kila siku kukiwa na taarifa za HIV katika vyombo vya habarikutasaidia kukumbusha jamii kuendelea kuchukua  tahadhali

Mapema  Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Arusha,Brandina Nkini ametoa taarifaya maambukizi ya HIV yanavongezeka  jijini Arusha kutoka 1.6 mwaka2007 hadi kufikia3.2 mwaka  2012..

No comments:

Post a Comment