Thursday, November 28, 2013

WALEMAVU MARA WAOMBA KUSHIRIKISHWA KATIKA VIKAO VYA MAAMUZIMUSOMA

Baadhi ya  Walemavu katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara wameomba  kushirikishwa katika Vikao mbalimbali vya Maamuzi Mkoani humo kama njia ya Kupanga na kushauri mambo yanayowahusu  watu wenye ulemavu katika Maisha yao ya kila siku.

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Mkoa wa Mara (CHAWATA) Bw Yohana Magai  katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho ambao ulikuwa ni Maalum kuchagua viongozi wa Chama hicho.Mwenyekiti huyo pia aliomba kutengwa kwa fedha ambazo zitasaidia kuendesha mambo mbalimbali yanayowahusu na kuwepo takimu sahihi za watu wenye ulemavu hapa nchini ambapo kwa Mkoa wa Mara idadi ya Walemavu wa Viungo ni 8,856.

“Nasi tunapaswa kupewa Mafungu ambayo yatatusaidia katika kuendesha shughuli zetu na kujua takwimu sahihi za Walemavu hapa nchini na kwa kufanya hivyo naamini Serikali itajua jinsi gani ya kutusaidia” alisema Mwenyekiti Magai

Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za CHAWATA Mkoa wa Mara kwa kipindi cha miaka Mitano 2008-2013  Katibu wa Chama hicho Bw Leonard Lameck alisema kuwa katika kipindi hicho Chama kimeweza kuwa na Ofisi kwani hilo lilikuwa tatizo kubwa tangu kuanzishwa kwa Chama hicho Mwaka 1982.

 “Kutokuwa na ofisi ilikuwa ni Changamoto kubwa kwa Chama chetu lakini tunashukuru tangu tumeingia Madarakani tumeweza kufanikisha kupatikana kwa ofisi nah ii ni tangu kuanzishwa kwa chama hiki mwaka 1982: alisema Katibu huyo.

Aidha katika taarifa hiyo,Chama hicho kililipongeza Shirika la The Foundation for Civil Society la jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa zaidi ya shilingi milioni 40 ambazo zilitolewa na Chama hicho katika kuendesha mambo mbalimbali ya Chama hicho
                    Baadhi ya Wajumbe katika Mkutano Mkuu wa CHAWATA MARA
Pamoja na Taarifa hiyo kuonyesha Mafanikio katika kipindi cha Miaka mitano lakini pia Chama hicho bado kinahitaji Msaada mkubwa katika kuendeleza kazi za Chama hicho ikiwemo kuelimisha Jamii ya watu wenye ulemavu.

 ‘Bado tuna Matatizo makubwa sana katika Chama chetu ili tufikie Malengo lazima tupoate wafadhili mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi”alisema Bi
Leonard

Changamaoto nyingne ambazo zilielezwa katika taarifa hiyo ni pamoja na kutokuwepo kwa vyanzo vya Mapato,ukosefu wa kadi za Wananchama,ukosefu wa vyenzo vya kujongea na vifo ambapo katika kipindi cha Miaka mitano viongozi watano wa CHAWATA Mara walifariki duni kutokana na magonjwa mbalimbali.

Akifungua  Mkutano huo Bi Magreth Munduli ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mara aliwataka Watu wenye ulemavu kufanya kazi kwa ukaribu na ofisi za Serikali ili wasione kama wanabaguliwa katika Mambo mbalimbali ya Maamuzi

Alisema watu wenye ulemavu wamekuwa na Changamoto nyingin lakini wao kama watendaji watajitahidi kuwasaidia ili wawe katika Mazingira bora.

 “ Tunajua Mnachangamoto nyingi lakini kama ofisi tunajitahidi kupambana nazo ili msione kama mnabaguliwa lakini pia andikieni Maandiko yetu na mmpelekee Mkurugenzi ili bajeti ikiwa inapangwa nanyi mtazamwe” alisema Bi Magreth Mundulu

Katika Mkutano huo wanachama walimchagua Bw Yohana Magai kuendelea na nafasi ya Mwenyekiti na Leonard Lameck nafasi ya Katibu huku nafasi wa Mweka hazina ikienda kwa Lucyiana Daudi ambapo watakaa katika nafasi hizo kwa kipindi cha Miaka mitano

No comments:

Post a Comment