Saturday, November 23, 2013

PROFESA BAREGU, MARANDO MAJI YA SHINGO, WAACHIA NGAZI CHADEMA


Wakati hali ikiendelea kutafsiriwa kuwa tete, katika CHADEMA  baada ya uamuzi wa chama hicho kumpiga chini aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe pamoja na wenzake wawili, jana,  hali imezidi kuwa ya majanga zaidi ndani ya chama hicho, kufuatia Mjumbe wa Tume ya Katiba, Profesa Mweisiga Baregu na Mabere Marando, kutoa kauli ya kujiondoa na kujiuzulu nafasi zao ndani ya Chama hicho.

Habari zinasema, Profeasa Baregu (pichani) na Marando ambao amekuwa chachu ya maana sana katika Chadema, wamefikia uamuzi huo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na kikao cha Kamati kuu ya chama hicho.

Huyu ni Mjumbe wa pili wa Kamati Kuu ya Chadema kuamua kujiuzulu wadhifa wake katika kipindi kisichozidi saa 12. Taarifa zaidi zitakuja baadaye

No comments:

Post a Comment