Monday, September 9, 2013

Volcano kubwa duniani yagunduliwa chini ya bahari, ina ukubwa wa saiz ya Ubelgiji (Belgium)

Volcano yenye ukubwa wa Ubelgiji (Belgium) imegunduliwa kwa mara ya kwanza, na jopo la wanasayansi  chini ya bahari ya Pacific. wanasayansi hao, wamegundua kuwa mwamba huo mkubwa ulitokana na mlipuko wa lava, na kuifanya volcano hiyo mpya kuwa sio tu ni kubwa duniani, bali ni kubwa katika solar system-kubwa kuliko Olympus Mons  (iliyoko mars.)

Tamu Massif Iko juu ya plateau kubwa iliyoko Km 2 chini ya maji, kaskazini-kusini  mwa bahari ya pacific ya mashariki ya Japan,volcano hiyo yenye ukubwa wa sq Km 310,000 (119,000 sq m) haina madhara wanasayansi hao wamesema. Mara ya mwisho kuripuka ilikuwa ni chini ya maji, miaka milioni 142 iliyopita wakati wa kipindi cha mwisho cha Jurassic, kabla binaadam kuumbwa
Utafiti uliochapishwa  katika "Nature Geoscience unaonyesha kuwa formation zaidi  ya miamba mikubwa chini ya maji inaonekana kuwa ni matokeo ya volcano kubwa zilizokufa zamani.

No comments:

Post a Comment