Sunday, July 14, 2013

BARABARA YA BALILI MANCHIMWERU YAKARABATIWABaadhi ya wananchi wa Vijiji zaidi ya 10 vinavyopitiwa na barabara ya Balili Manchimweru wilaya ya Bunda mkoani Mara wameipongeza Serikali kwa kuipandisha hadhi barabara hiyo kuwa chini ya TANROAD na pia kuitengeneza kwa kiwango cha Changalawe.

Sauti za wananchi hao zimesikika mbele ya waandishi wa habari wakati wa Matengenezo ya barabara hiyo yenye urefu wa km 41 kupitia Kampuni ya ukandarasi ya Keres Tanzania LTD.  

Wamesema kabla ya ujenzi huo barabara hiyo ilikuwa kero hasa nyakati za Mvua lakini kukamilika kwa barabara hiyo  kutarahisisha mambo mengi katika maisha yao ya kila siku

Kwa upande wake Fundi Mchundo wa barabara  hiyo Bw Charles Joseph  amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilling Milion 300 ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi sita lakini kutokana na Mvua zilizokuwa zikinyesha ulichelewa kukamilika na hivyo kukamilika mwishoni mwa mwezi julai.Kutengenezwa kwa barabara hiyo kunafuatia malalamiko ya Mara kwa Mara ya Wananchi hao hasa nyakati za Mvua na hivyo kutengezwa kwa kiwango cha Changalawe ni faraja kwa wakazi wa Vijiji hivyo

No comments:

Post a Comment