……………………………………………………..
Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika
ya mashariki Dr. Richard Sezibera amefungua rasmi kongamano la
waandishi wa Habari Tanzania pamoja nchi wanachama wa jumuiya ya afrika
ya mashariki katika kuadhimisha ya uhuru wa vyombo vya Habari Diniani
uliobeba kauli isemayo USALAMA NA MAZINGIRA BORA YA KUFANYIA KAZI KWA
WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI AFRIKA YA MASHARIKI.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kaongamano hilo la waandishi wa habari liliofanyika jijini hapa katika
ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Naura Spring amesema kuwa kongamano
hili la vyombo vya Habari pamoja na wamiliki lina umuhimu kwa sababu
litaifanya jamii pamoja na serikali kujua nini umuhimu wa uhuru wa
vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi na jamii yote.
Amesema kuwa uhuru wa vyombo vya
habari kwa kiasi kikubwa unajikita katika uhuru wa kutoa maoni na pamoja
na uhuru wa kutoa habari hivyo katika kuelewa hilo vyombo vya habari
vinatakiwa viwe vinafanya kazi zake pasipo kuegemea upande wowote ili
kusije kuchochea kuvunja amani ya nchi kama ilivyotokea miaka ya nyuma
kwa nchi ya Rwanda na Burundi.
Aidha amesema kuwa kuna changamoto
kubwa sana zinazovikumba vyombo vya habari hususani vyombo vya kijamii
ambapo wanakuwa na mazingira magumu ya kutafuta habari na kufanya
wakati mwingine waandishi kuwa katika mazingira hatarishi kwa maisha
yao pamoja na hali mbaya ya kiuchumi inayopelekea kutoweza kufanya kazi
kuendana na mabadiliko ya sayansi na Technolojia ikiwepo kujiingiza
katika mawasiliano ya mkongo wa kimtaifa.
Kongamano la mwaka huu
limeratibiwa na MISSA TANZANIA kwa kushirikiana na EAJA, Mfuko wa
vyombo vya Habari Tanzania ( TMF), Muungano wa klabu za wandishi wa
habari (TPC), Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania, Baraza la Habari
Tanzania (MCA), Wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini (MOAT) pamoja na
kituo cha habari kwa wananchi TCIB.
No comments:
Post a Comment