Tuesday, April 16, 2013

WAWILI WAJINYONGA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI MUSOMA


WANAWAKE wawili katika  Manispaa ya Musoma maeneo tofauti  wamejinyonga  huku mmoja akijinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruali na mwingine akijinyonga kwa kutumia  mtandio wa nguo yake
Katika tukio la kwanza mwanamke  aitwaye Rudia kyango umri wa miaka 40 Mkazi wa kata ya Kigera  Manispaa ya Musoma  amekutwa amekufa kufuatia kujinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruali na kuleta simanzi kubwa kwa familia yake.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia april 13 mwaka huu ambapo marehemu alijinyonga kwa  kutumia mkanda wa suruali na kufariki dunia na mara baada ya wakazi wa eneo hilo kufika nyumbani kwa marehemu walitoa taarifa  katika kituo kidogo cha polisi kigera  na polisi kuuchukua mwili wa marehemu kwa  kwaajili ya uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya mkoa wa mara.

Wakati huo huo Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama marwa  Mkazi wa Mtaa wa Ghandhi  manispaa ya musoma anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 27 hadi 30 amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio wa nguo yake akiwa chumbani.

Tukio hilo limetokea asubuhi  leo (jana)  katika mtaa wa ghandi mjini Musoma baada ya watoto wake kwenda shuleni  ambapo majirani walimshuhudia na kutoa taarifa polisi.

Majirani hao waliiambia blog hii Mwanamke huyo huenda alichukua maamuzi hayo baada ya watoto wake kwenda shuleni na kubaki pekee yake nyumbani.

wamekumbana na mama huyo akiwa amejipiga kitanzi shingoni kwa kutumia mtandio wa nguo na kufariki dunia.
Umati wa wakazi wa Manispaa  ya Musoma ulijaa katika eneo la tukio  huku simanzi zikitawala kufuatia kifo hicho cha kujinyonga  ambapo  marehemu kabla ya kifo chake alikuwa anafanya kazi kwa mtu binafsi ya kuuza  vinywaji baridi.

Jeshi la polisi  lilifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwaajili ya uchunguzi  wa  kitabibu na pia kuchunguza kubaini  kilichopelekea kifo cha marehemu huyo.
 
Source: Shomm Binda

No comments:

Post a Comment