Tuesday, April 16, 2013

Serikali yaunda kamati maalumu kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa StarsWaziri wa Habari,

Utamaduni na Michezo

Fenella Mkangara.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri kwenye michezo yake iliyobakia ya kufuzu michuano ya Kombe la dunia 2014.

Hivi karibuni Stars ilifanikiwa kuifunga Morocco mabao 3-1 hivyo kufanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi C walilopo wakiwa na timu zingine za Ivory Coast na Gambia.
Msimamo wa kundi hilo mpaka sasa Stars wako katika nafasi ya pili wakiwa na alama sita, nyuma ya vinara Ivory Coast wanaoongoza kwa alama saba na Morocco ni ya tatu wakiwa na alama mbili wakati Gambia wao wanashikilia mkia wakiwa na alama moja. 

Kutokana na matokeo hayo wizara kupitia waziri wake Fenela Mukangara wameipongeza timu hiyo kwa kuweka matumaini hai ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014, na kwa kuzingatia hilo wizara imeamua kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kuongeza hamasa ya ushindi kwa Stars ili iweze kuweka historia kwa kushiriki michuano ya Brazil.
Jukumu la msingi la Kamati iliyoundwa ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi.
Wajumbe wa Kamati ya Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa wafuatao:-

Bw.Mohamed Dewji - Mbunge

Bi. Teddy Mapunda - Montage

Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF

Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT

Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel

Bw. George Kavishe - TBL

Bw. Mohamed Raza - Zanzibar

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Bw. Joseph Kusaga - Clouds

Bw. Kapt. John Komba - Mbunge

Bw. Zitto Kabwe - Mbunge


Kamati hiyo iliyoteuliwa leo(April 16,2013), inatakiwa kuanza kazi kazi mara moja. 
Hadidu za rejea zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Kamati itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa. Serikali inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele yetu.

No comments:

Post a Comment