Monday, April 15, 2013

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) WAPELEKA MADAKTARI BINGWA KIGOMA, WAGONJWA WAMIMINIKA

1
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kigoma, Ramadhan Maneno akifungua rasmi mpango wa NHIF wa madaktari bingwa kutoa huduma katika hospitali ya Rufaa Maweni.
2
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee akikabidhi vifaa na dawa zitakazotumiwa na madaktari hao kwa muda wa siku saba kwa uongozi wa Mkoa.
Uongozi wa Mkoa, NHIF na Madaktari bingwa wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kuanza kazi ya kuona wagonjwa.
E80A5148
Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma akitoa neon la shukurani kwa mpango huo wa NHIF
E80A5184
Kaimu Mkuu wa Mkoa akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa mkoa muda mfupi baada ya kupokea kutoka kwa uongozi wa NHIF

Na Grace Michael, Kigoma

Mamia ya wagongwa mkaoni Kigome wamejitokeza kuonana na jopo la Madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa ya Mhimbili waliopelekwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF ambao unaendesha mpango wa kuwapeleka madaktari hao mikoa mbalimbali ya pembezoni mwa Tanzania.

Mpango huo wa NHIF una lengo la kuwasaidia wanachama wake pamoja na wananchi wa kawaidia kupata huduma za wataalamu hao wakiwa maeneo yao hivyo kuepuka kufuata huduma zao jijini Dar es salaam au Mwanza.

Akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa ya Maweni mkoani Kigoma, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Ramadhan Maneno amesema kuwa kitendo cha NHIF kupeleka madaktari hao ni cha kupongezwa kwa kuwa kina lengo la kuokoa maisha ya wananchi na kupunguza gharama pia kusaidia kuboresha huduma katika maeneo husika.

“Uongozi wa NHIF umefanya maamuzi ya busara kuwaleta madaktari hawa, nafarijika sana kuona wagonjwa wetu wanapata huduma zao, leo hii nimearifiwa kuwa zaidi ya watu 250 wamejitokeza kupata tiba, hii inatupa matumaini kuwa watu wamekubali na wengi zaidi watakuja kupata tiba ya wataalamu hawa”. Alisema Maneno.

Naye Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Hamis Mdee akitoa maelezo ya awali kabla ya madaktari hao kuanza kazi rasmi,  alisema kuwa kutokana na matatizo makubwa ya upatika na jiwa wataalam hasa katika mikoa ya pembezoni, mfuko umeanza utaratibu wa kuwapeleka madaktari bingwa katika mikoa hiyo na kutoa huduma na hasa za upasuaji.

“Mpango huu ni endelevu, tumeamua kufanya hivi ili kila mkoa uweze kunufaika na huduma hizi ambazo si rahisi kuzipata, pia itawasaidi watumishi wa hospitali watakazokuwepo kupata ujuzi zaidi kutoka kwa madaktari bingwa”. Alisema Mdee.

Aidha Mdee hakusita kuwaeleza wananchi wa Kigoma umuhimu wa kujiunga na mfuko wa Bima ya afya kwani unamsaidia mgongwa kupata tiba hata kama hana fedha.

Mbali na NHIF kupeleka jopo la madaktari hao pia wamepeleka vifaa vifaa vitakazyotumika wakati huu wa huduma hizo.
Madaktari bingwa walioko Mkoani hapa kwa ajili ya kutoa huduma ni pamoja na Dk.Makia, Dk. Mrema, Dk. Kisengena Dk. Sakwari.
Mikoa mingine inayotarajiwa kufikiwa na mpango huu ni Rukwa, Katavi na Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment