Wednesday, April 17, 2013

"WAISLAMU PEKEE NDO WARUHUSIWE KUCHINJA NYAMA YA BIASHARA"....HII NI KAULI YA LEO YA RAIS MWINYI


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) aliowaita leo nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam,wakati alipozungumzia swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.Mzee Mwinyi ametoa rai kuwa Swala hilo ambalo limekuwa na utata mkubwa na kupelekea kuzua vurugu kwa baadhi ya maeneo hapa nchini,kuwa liachiwe watu wenye dharura kama linavyoelekeza kwenye Moja ya Vitabu vya dini.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wamsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

 Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya waandishi wa Habari waliofika nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment