Emanuel Bwimbo kulia akiwa na Anna Mroso katika mkutano na Mwenyekiti wa CCM
Shomar Binda akiwa katika pozi
MUSOMA
Chama cha
Mapinduzi mkoani Mara kimesema hakipo tayari kuwa na kiongozi ambaye hatimizi wajibu wake kwa Wananchi na hivyo kupelekea Wananchi kulalamika juu ya
Serikali iliyopo Madarakani.
Kauli hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mara Bw. Christopher
Mwita Sanya wakati akiongea na Waandishi wa habari mkoani hapa.
Amesema
wabunge na Madiwani wa Chama hicho waliochaguliwa katika uchaguzi Mkuu mwaka
2010,Sanya amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kutimiza kile walichokiahidi
wakati wa Kampeni.
Kuhusu suala
la Makundi ndani ya Chama hicho Mwenyekiti huyo amesema kwasasa suala hilo halina
nafasi huku akieleza sababu ya kufanya vibaya Kwa baadhi ya Maeneo katika uchaguzi
Mkuu uliopita.
Katika hatua
nyingine Bw Sanya amewataka Vijana kutochagua kazi na kuamini Kilimo kama njia
sahihi kufanikiwa katika Maisha.
No comments:
Post a Comment