Thursday, April 18, 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KWENYE MAZISHI YA BI. KIDUDE

9
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Msanii mkongwe wa Muziki wa Mwambao (Taarab) Tanzania,Marehemu Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja jana.

MH. DKT. KIKWETE AONGOZA MAZIKO YA KAKA YAKE MAKAMO WA RAIS DK. BILALI


Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu
wakilibeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Haji Gharib Bilali,mdogo
wake Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Mohammed Gharib Bilal,kabla ya kuswaliwa katika msikiti wa Kilimani
Mjini Unguja leo na kuzikwa Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_9822 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,(kushoto waliosimama) Rais wa Jamhuri ya
Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamo wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano,Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,pamoja
na wananchi wakiwa katika maziko ya Haji Gharib Bilali,mdogo wake
Makamo Dk.Bilal,yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi
Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_9828 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,,akitia udongo katika kaburi la
Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo  wake Makamo wa Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa
maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi
Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_9832 
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete,akitia udongo katika kaburi la   Marehemu Haji Gharib Bilali,
Mdogo  wake Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika leo
jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.] IMG_9842 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
  Dk. Ali Mohamed Shein,,akitia udongo katika kaburi la
Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo  wake Makamo wa Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa
maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi
Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

source Fullshangwe

No comments:

Post a Comment