Monday, April 29, 2013

Siku ya Mashujaa Kitaifa mwaka huu kufanyika mkoani KAGERA,Kanali MASSAWE aitaka Jamii kushiriki kikamilifu.

Kanali Fabian Massawe.
Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE, ameshauri vyombo vya habari na Wana habari kuhamasisha jamii mkoani humo kujiandaa kikamilifu  kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa.



Kanali mstaafu MASSAWE ametoa kauli hiyo mkoani Kagera alipokutana na wakurugenzi na waandishi wa vyombo mbalimbali pamoja na wadau wa habari mkoani humo.
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa  hufanyika  kila tarehe 25 mwezi Julai.
Kitaifa mwaka huu  yatafanyika Julai 25, mkoani KAGERA, katika kambi ya Jeshi la Wananchi-JWTZ-KABOYA, wilayani MULEBA.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo  atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk JAKAYA KIKWETE.

Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE, ameshauri vyombo vya habari na Wana habari kuhamasisha jamii mkoani humo kujiandaa kikamilifu  kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa.

Picha juu na nichi ni baadhi ya waandishi habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia katika mkutano huo uliowashirikisha wadau wa habari pia.


Kanali MASSAWE amesema  vyombo vya habari na Wanahabari  ni kiungo muhimu katika kuhamasisha jamii iweze kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo.
 
Ameshauri Wazee walioshiriki matukio  wakati ule kujitokeza na kusimulia  ili liwe fundisho kwa   jamii ya sasa itambue uzalemdo wa kuipigania nchi yao.
 
Aidha amewataka Wakazi wa mkoa wa KAGERA kutumia fursa hiyo kuwekeza zaidi na kupata ajira.

No comments:

Post a Comment