RAIS wa Jamhuri ya Muungan wa Tanzania Dk. Jakaya Mrsho Kikwete amemteua Mh. Mwantumu Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huo wa Mahiza umeanza Aprili 19 mwaka huu.
Balozi Sefue amesema Mh. Mwantumu Mahiza atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne hadi Aprili 19 mwaka 2017.
Mh.
Mwantumu Mahiza anakuwa Skauti Mkuu kuchukua nafasi ya Kanali Mstaafu
Idd Kipingu aliyemaliza muda wake kutumikia nafasi hiyo.
Mh. Mahiza mbali na kushika wadhifa huo, pia anatumikia nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA KILIMO.
Na Hassan Silayo na Lorietha Laurence
…………………………………………………….
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete anatarajia kufungu
a mkutano wa Kilimo wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Africa, utakaofanyika tarehe 13 hadi 14 Mei mwaka huu .
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkutano wa Vyama vya Kilimo vya
Kusini mwa Afrika (SACAU), Ishmael Sunga wakati akiongea na waandishi
wa habari kuhusu mkutano huo utakao fanyika katika hoteli ya White sands
iliyopo jijini Dare s salaam.
Alisema kuwa kipaumbele katika kipindi hiki ni kupambana na changamoto ya kilimo,na usalama wa chakula ili kufanya sekta ya kilimo kukua , kustawi na kufanya kilimo kuwa biashara badala ya kufikiri katika kuondoa umaskini.
“Lengo
litakuwa ni kubadilisha mtazamo wa watu kuwa, kilimo ni kwa ajili ya
kumfanya mkulima ajikimu mahitaji ya kawaida na kuondoa umaskini, bali
ni kumfanya mkulima kupata faida na kutajirika kupitia kilimo katika
ngazi zote za kilimo”, alisema Sangu.
Aliongeza
kuwa mkutano huo una malengo ya kuwasaidia na kuwaongezea nguvu
wakulima pamoja na kutoa taarifa za kilimo kwa wadau wa sekta hiyo kwa
niaba ya wakulima wote wanachama wa umoja huo ili kuleta tija katika
sekta hiyo muhimu ya kilimo.
Naye
Mkurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania Janet Bitegeko alisema baada ya
mkutano huo washiriki watapata fursa ya kutembelea wakulima wa mpunga
katika kijiji cha Bagamoyo ili kujionea changamoto na nini wakulima hao
wanafanya na kutoa ushauri ili kuweza kuboresha zaidi zao hilo.
Janet aliongeza kuwa umoja huo utatoa taarifa za utekelezaji za mwaka pamoja na kufanya ukaguzi wa hesabu za mwaka za umoja huo.
Mkutano
huo utahudhuriwa na washiriki kutoka nchi 14 wakiwemo wakurugenzi na
wenyeviti kutoka nchi za kusini mwa afrika, wawakilishi zaidi ya 10 wa
muungano wa wakulima pamoja na taasisi za kifedha.
Kauli
mbiu ya mkutano huo ni kusaidia kilimo cha biashara na maendeleo ya
biashara yanayolenga mkakati maendeleo ya kilimo katika nchi za kusini
mwa afrika, ambapo waziri wa kilimo wa Nigeria atatoa kauli.
Wanajeshi kutoka nchini Nigeria waitembelea wizara ya Habari
Katibu
Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
(kulia) akiangalia picha ya nembo ya chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha
nchini Nigeria aliyopewa na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini
Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake
leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo hicho wako
nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.PICHA NA ANNA NKINDA WA
MAELEZO Mkurugenzi
wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John
(kushoto) akimwelezea Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda kuhusu picha ya kinyago
kinachoonyesha mtawala wa makabila mbalimbali ya nchi hiyo
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya
wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria
wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano. Katibu
Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
(kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji
kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea ofisini kwake
leo jijini Dar es Salaam. Katibu
Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
(kulia) akimkabidhi picha ya kinyago cha ujamaa Mkurugenzi wa kikosi
cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati
wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea
ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao kutoka nchini
Nigeria wako ziara ya mafunzo ya siku tano nchini.
Kanali Anderson Msuya (kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania
(JWTZ) akiongea jambo na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini
Nigeria Meja Generali Ati John wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha
Ukamanda na Unadhimu walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Mchezo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini
Nigeria wakimsikiliza Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati
walipomtembea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu
kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu
cha nchini Nigeria walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi msaidizi Idara ya utamaduni. Wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar
es Salaam. Wanajeshi hao kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako
nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
JAJI MKUU WA TANZANIA AMTEMBLEA SPIKA WA BUNGE OFISINI KWAKE DODOMA LEO
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alipofika kumtembelea Ofisini kwake Dodoma leo na kufanya nae mazungumzo.(PICHA ZOTE NA OWEN MWANDUMBYA WA BUNGE)
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alipofika kumtembelea Ofisini kwake Dodoma
Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake
wakimsikiliza Spika wa Bunge Ofisi Kwake leo. Jaji Mkuu na Ujumbe wake
walimtembelea Mhe. Spika na kufanya nae Mazungumzo Ofisini kwake Mjini
DodomaMbunge wa Maswa (CHADEMA) Mhe. John Shibuda akimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman kuelekea Ofisi ya Spika alipofika viwanja vya Bunge leo. Jaji Mkuu na Ujumbe wake walimtembelea Mhe. Spika na kufanya nae Mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma
Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde akieleza jambo kwa hisia Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman katika viwanja vya Bunge leo.Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisalimiana na Mhe. Ngeleja Bungeni leo
KAMUHANDA -ELIMU YA UZALENDO IMECHANGIA NCHI KUWA NA AMANI NA UTULIVU Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akisoma jarida la Eagle alilopewa Zawadi na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati
John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini
Nigeria wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
…………………………………………………………….
NA MAGRETH KINABO
ELIMU
ya uzalendo imesaidia kuwafanya vijana wa Kitanzania kuipenda nchi
yao , hali iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana
,Utamaduni na Michezo,Seth Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa
watu 22,baadhi yao ni viongozi wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha
Ukamanda na Unadhimu wa mafunzo ya kijeshi kutoka Nigeria.
Ujumbe
huo umetembelea wizara hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali
ya Utamaduni wa Kitanzania, umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja
Generali, Ati John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo
ya program tunazowafundisha vijana ili kuondoa migogoro katika nchi
yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda nchi
yao. Elimu hii imesaidia kupunguza migogoro,alisema.” Katibu Mkuu huyo
alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi hao lililouliza kuwa
kuna program zipi zinazochangia kupunguza migogoro hususan kwa
vijana.
Katibu
Mkuu huyo aliongeza kuwa kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi
ili waweze kubuni miradi mbalimbali kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo vijana wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli mbalimbali kuwawezesha kiuchumi.
Aidha
Katibu Mkuu huyo akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema
wizara yake ndi yenye jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo
katikawizara hiyo yenye sekta nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo.
Kamuhanda alisema sektaya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
Aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini na ndiyo iliyoleta umoja ,amani na mshikamano.
Wakizungumzia
kuhusu ziara hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi, Ikema Francis
walisema wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya
kiutamaduni na kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.
No comments:
Post a Comment