Wednesday, May 1, 2013

OFISA MTENDAJI ALIYEGUSHI NA KUIBA SH,MIL.10 AKATALIWA NA KIJIJI.

SERIKALI ya kijiji cha Monuna kata ya Nyambureti wilayani Serengeti Mkoani Mara imemkataa ofisa mtendaji wa kijiji hicho John Ntora baada ya kubainika kushirikiana na mkandarasi kuiba sh,mil.10 za ujenzi wa nyumba ya waganga.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Juma Watanda amesema,katika kikao cha aprili 25,mwaka huu wamefikia uamzi huo kwa kuwa wananchi hawana imani naye.
Amesema pia uamzi huo unalenga kunusuru maisha yake baada ya wananchi kutishia kumshambulia ,kufuatia mwajiri wake licha ya kujua wizi huo hajachukua hatua yoyote ikiwemo kumtaka apishe ofisi kwa ajili ya uchunguzi.
Akiongea na blogu hii ofisa mtendaji huyo amekiri kukataliwa na serikali ya kijiji na kuwa kwa sasa yuko kijijini kwao Maburi akisubiri hatima yake kutoka Takukuru na mwajiri..
Amekiri kugushi mhutasari wakishirikiana na Solomoni Nkaina ambaye alikuwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya waganga na kuchukua sh,mil,17 badala ya sh,mil,10 zilizoidhinishwa kamati ya ujenzi ya kijiji hicho.
Na kuwa yuko tayari kulipa kiasi hicho cha fedha ili mambo yaishe,”nimekubali kulipa ingawa mwennzangu alikimbia na fedha zote mpaka sasa….unadhani mimi nitafanyaje kama mambo yameishakuwa hivyo”amesema Ntora.
Septemba 19,2012 ofisa mtendaji huyo kwa kutumia muhtasari K/U/K/M./VOL10/012 wa agosti 20,2012 ulioidhinisha sh,7,890,000=  kwa ajili ya kumlipa kampuni ya J.N.L Construction and General Traders Ltd,inayojenga nyumba hiyo kwa gharama ya sh,mil.34 chini ya mpango wa MMAM.
Hata hivyo ofisa mtendaji huyo alimwandikia msimamizi wa mradi huo kwa jina lake Solomon Eliud Nkaina badala ya kampuni na kuongeza tarakimu hivyo kusomeka sh,17,890,000= na kufanikiwa kuchukua kwenye akaunti namba 3026600268 na kubakiza sh.16,972,292= 
Kutokana na tuhuma hizo Takukuru wilayani hapa wanaendelea na uchunguzi baada ya kumkamata na kumhoji.

No comments:

Post a Comment