Wednesday, March 6, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA MUSOMA


003Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo na kuoneshwa Ramani za ujenzi wa nyumba za watumishi wa Umma, wakati Makamu alipofika eneo hilo kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa nyumba hizo jana Machi 5, 2013. Picha na OMR 004Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBA, mara baada ya Makamu kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Umma, jana Machi 5,2013. Picha na OMR 005Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Musoma Mjini Mkoa wa Mara, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mukendo jana Machi 5, 2013 ikiwa ni siku ya mwisho ya zaiara yake mkoani Mara. Picha na OMR
Msondo 4Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Kushoto ni wanamuziki wa bendi hiyo, wakimshabikia. Picha na OMR Msondo2Wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakionyesha umahiri wao wa kupuliza ‘midomo ya bata’ wakati wa  bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment