Friday, March 8, 2013

MAAFISA WA POLISI NA USALAMA WA TAIFA WALIOKUTWANWAKICHIMBA DHAHABU HIFADHINI WAPANDISHWA KIZIMBANI

Na Mwandishi wetu- Machi 7,2013.
MUSOMA.

HATIMAYE maafisa  wa polisi na usalama wa Taifa waliokutwa wakichimba
dhahabu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara  wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mara  wakikabiliwa na makosa 6 ya uhujumu uchumi.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni karibu mwaka mzima toka wamekamatwa katika tukio hilo lililohusisha raia watano ambao walifikishwa mahakamani baada ya siku 2 toka wamekamatwa,huku maafisa hao wakihamishwa vituo vya kazi.

Waliofikishwa mbele ya mahakama hiyo ni SSP Paulo Cathbert
Mng’ong’o(56)aliyekuwa Ocd Serengeti,Said Mussa(44)aliyekuwa ofisa usalama wa Taifa na dreva wa polisi E 933 koplo  Frematus
Fredrick(42).

Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wakili wa serikali Valensi Mahenga
mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Emmanuel Loitare Ngigwana walitenda makosa hayo machi 24,2012 katika eneo la kilima fedha ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wakili huyo aliyataja makosa yanayowakabili kuwa ni kula njama kwa
lengo la kufanya kosa na kutenda kosa ,kuingia hifadhini kinyume cha sheria.

Makosa mengine ni kukutwa na silaha ndani ya hifadhi kinyume cha
sheria ,kufanya uchimbaji wa dhahabu ndani ya hifadhi ya taifa kinyume cha sheria,kupatikana na dhahabu ambayo haijasafishwa kinyume cha sheria na kukutwa na zana za milipuko ndani ya hifadhi kinyume cha sheria.

Washitakiwa wamekana mashitaka na wako nje kwa dhamana na kesi hiyo
itatajwa machi 19 mwaka huu.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limemfukuza kazi aliyekuwa dreva wa
  polisi koplo Frematus Fredrick mwenye namba  E 933 huku aliyekuwa  SSP Mng’ong’o  akiwa amesimamishwa kazi kutokana na cheo chake.

Katika tukio hilo maafisa hao pi a walikamatwa na raia watano

walioingia nao ndani ya hifadhi kwa ajili ya kutenda uharifu huo ambao tayari walishafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Serengeti.

Washitakiwa wengine ambao ni raia walifikishwa mbele ya hakimu wa
mahakama ya wilaya Amon Kahimba machi 26,2012 wakikabiliwa na makosa 5 huku kwa upande wa maafisa hao ikidaiwa kuwa uchunguzi na taratibu za kijeshi zilikuwa zinaendelea.

Makosa hayo ikiwa ni  kuingia ndani ya hifadhi ya Taifa bila

kibali,kupatikana na silaha bila kibali,kufanya uchimbaji wa dhahabu ndani ya hifadhi bila kibali na kupatikana namifuko 10 mawe ya madini ya dhahabu kinyume cha sheria. Kosa lingine likiwa ni kukutwa na vifaa vya milipuko ndani yahifadhi
.
Washitakiwa hao ni Mniko Nyamhanga Mwita (30)mkazi wa Matare,Jonas Marwa Chacha (42)mkazi wa Mugumu mjini,Maiga James Maganjala(26)mkazi wa Bunda . Wengine ni Mwita William King’eti(30)mkazi wa Mugumu na Alex Peter(29)Mwalimu wa sekondari Kambarage iliyoko mjini Mugumu

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi aprili mwaka huu baada
ya upande wa mashitaka kudai upelelezi umekamilika.

No comments:

Post a Comment