Monday, February 4, 2013

Watatu wauawa kikatili katika wilaya za Tarime na SerengetiMusoma

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti yakiwemo ya kuawa,kujinyonga na kuchomwa kisu mkoani Mara.
Katika tukio la kwanza lilotokea juzi watu wenye hasira katika kijiji cha Nyabirekera wilayani Serengeti,wamemuawa mkazi mmoja wa kijiji hicho kwa kipiga mawe kisha kuuchoma moto mwili wake baada ya kumtuhumu kujihusha kwa imani za kishirikina.


Kamanda wa polisi mkoani Mara,kamishna Msaidizi Mwandamizi Absalom Mwakyoma,alimtaja marehemu kuwa ni Nyabuke Maheri,ambaye anakisiwa kuwa na umri wa miaka 68.Hata hivyo kamanda Mwakyoma,alisema ingawa bado chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa lakini ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake wanapowakamata wahalifu kwa makosa yoyote wawafikishe katika vyombo dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.


Katika tukio lingine ambalo limetokea wilayani Tarime,kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya Justus Kamugisha,alisema mtu mmoja Genkuri Chacha(34) aliuawa baada ya kuchomwa kisu na mdogo wake Nyengwe Chacha(25).

No comments:

Post a Comment