Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa
MUSOMA
Serikali mkoani Mara imewataka wanasiasa waache kutumia Jukwaa la siasa kuchochea chuki,vurugu huku wakihamasisha
wananchi kuvunja sheria za nchi.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa
wa Mara John Gabriel Tupa,wakati wa
kukabidhi piki piki 12 kwa wilaya nne za mkoa wa Mara ambazo zimetolewa na
Serikali kwaajili ya kusadia suala la ulinzi katika mradi wa ukaguzi wa tarafa.
Mkuu huyo wa Mkoa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati
ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Mara amesema viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo na viongozi wa madhebu ya dini watumie
nafasi zao kuhubiri upendo na amani
miongoni mwa jamii pamoja na kuheshimu sheria za nchi.
Mbali na kauli hiyo Mkuu huyo wa mkoa
amesema Mkakati wa Jeshi la Polisi ni kuzuia Uhalifu na Kujenga mahusiano na
Jamii na kuongeza kuwa Pikipiki hizo zisitumike katika matendo yasiyofaa.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi
wandamizi Absalom Mwakyoma,amesema piki piki hizo ni sehemu piki piki 164 za
ukaguzi wa tarafa kwa kuzuia uhalifu mradi ambao uliziinduliwa na mkuu wa jeshi
la polisi nchini IGP Said Mwema January 11 mwaka huu lengo likiwa ni kupambana
na wahalifu na uhalifu hapa nchini.
Wilaya zilizoweza kupata pikipiki hizo
ni wilaya za Serengeti,Bunda,Musoma mjini na wilaya ya Butiama
No comments:
Post a Comment