Thursday, February 7, 2013

TAZAMA STARS NA CAMEROON ILIVYOKUWA UWANJA WA TAIFA

Mbwana Samatta wa Tanzania akifunga bao baada ya kumlamba chenga kipa wa Cameroon, Efalla Komguep katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya timu hizo jioni ya leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tanzania, Taifa Stars ilishinda 1-0.

Beki wa Stars, Erasto Nyoni akimtoka beki wa Cameroon, Assou Ekotto

Thomas Ulimwengu akiwa ameruka juu na kipa wa Cameroon, Efalla Komguep kuwania mpira wa juu

Mbnwana Samatta akipambana na mabeki na kipa wa Cameroon

Kiungo Frank Domayo wa Tanzania kulia akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Cameroon, Nyom Allan

Wachezaji wa Tanzania wakishangilia bao lao lililofungwa na Samatta waliyemdandia

Wa Mazembe, si wazembe; Thomas Ulimwengu akimpongeza mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta kuifungia Stars leo 

Kikosi cha Cameroon leo

Kikosi cha Stars leo

Samatta akimfunga tela Ashu Clovis

Thomas Ulimwengu akiwalamba chenga mabeki wa Cameroon

Beki Shomary Kapombe akitia krosi huku beki wa Cameroon, Nyom Allan akiipisha

Beki wa Cameroon, Aminou Bouba akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto

Hapa ndipo Stars ilipopata penalti, beki Ngoula aliupitia mpira miguuni mwa Samatta akitokea nyuma ndani ya eneo la hatari

Beki wa Cameroon, Assou Ekotoo akimiliki mpira mbele ya kiungo Mrisho Ngassa wa Tanzania

Ekotto akimiliki mpira mbele ya Ngassa

Beki Pierre Wome wa Cameroon akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Samatta, huku  Ekotto kulia akiwa tayari kutoa msaada

No comments:

Post a Comment