Thursday, November 15, 2012

WAFANYABIASHARA KATIKA MANISPAA YA MUSOMA WALALAMIKIA ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMAMOTO


ASKARI WA ZIMAMOTO WAKIWA NA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPARESHENI YA KUKAGUA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO KATIKA MADUKA

OPARESHENI MTAANI

ASKARI WA ZIMAMOTO AKIZOZANA NA MWENYE DUKA

GARI LA ZIMAMOTO LIKIWA KATIKA OPARESHE 
Wafanyabiashara wa maduka yanayouza bidhaa mbalimbali katika Manispaa ya Musoma wameilalamikia Halimashauri ya Manispaa hiyo kitengo cha Zimamoto kwa kuwasulutisha kufunga maduka yao kwa kile kinachoelezwa oparesheni ya kuangalia maduka ambayo hayana vifaa vya kuzimia moto.

Wakizungumza na Blogu hii kwa nyakati tofauti Mjini Hapa,wamesema hawapingani na sheria ya kuwa na vifaa hivyo katika maduka yao lakini wanashangazwa na utaratibu unaofanywa na kikosi cha Zimamoto kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwalazimisha kufunga maduka yao na kukwamisha shughuli za Biashara.

Wamesema elimu inapaswa itolewe kuhusiana na matumizi ya vifaa hivyo na si kutumia nguvu kubwa na kulazimishwa kufungwa kwa maduka wakati wanalipia ushuru pamoja na mapato mengine ya kuendesha biashara zao.

"Huu tunajua ni mradi wa mtu pale  Manispaa na ndiye anaye toa amri ya kutumika kwa oparesheni hii ambayo si tunaona ni kero kwetu maana kama unavyoona maduka mengi yamefungwa kutokana suala hili,"alisema mmoja wa Wafanyabiashara hao.

Blogu hii ilifanya jitihada za kufika katika Ofisi za Manispaa ya Musoma ili kafahamu suala hili kwa kina lakini jitihada za kumpata muhusika wa kulizungumzia akuweza kupatikana.

No comments:

Post a Comment