Friday, November 23, 2012

KIWANDA CHA MGANGO GINNERY CHAENDELE KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI

 Hili ni bango linaloonekana katika Mlango wa kuingia kiwandani
 Hapa watu wanachakarika kiwandani ndani kazi hakuna kulala
     Tukiwa kiwandani na mwenyeji wetu B Joseph Mathayo tukauza sura kidogo mm na Shom B
    Hapa nikitazama moja ya Mashine ambayo ni mpya kiwandani hapo
   Mkurugenzi wa Kiwanda huyo Bw Joseph Mathayo akizidi kutupatia maelezo
            Safi kazi inaendelea
              Hapa tukiangalia Pamba ambayo tayari imeishwa tengenezwa yaani ni safi
              Tunazidi kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa ndugu Joseph Mathayo
                              Umakini unatakiwa wakati wa Maelezo
        Hapa ni sehemu ya kusaga Mbegu zilizochambuliwa
                               Jamaa wakaamua kuweka Pozi
               Si mbaya kuweka Pozi
                                Haya ni Mafuta ambayo yanazaliwa kiwandani hapo
                    Mashudu kwa ajili ya chakula cha Ngo'ombe
        Tulikuta baadhi ya Pamba safi ikiwa tayari na hili ni moja ya gari ambalo lilikuwa tayari kupakia kuelekea Jijini DSM
  Bw Joseph Mathayo (Rambo) ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda hicho

Augustine Mgendi

BUTIAMA

Kiwanda cha Pamba cha Mgango Ginnery kilichopo katika eneo la Mgango wilaya ya  Butiama Mkoani Mara kimeendelea kujenga Mahusiano Mazuri na Wakulima kutoka mikoa ya Mara,Mwanza na Simiyu kuwaendeleza katika zao la Pamba.

Akiongea na Waandishi wa habari waliotembelea kiwandani hapo,Mkurugenzi wa kiwanda hicho Joseph Mathayo  alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza uzalishaji mwezi Julai mwaka huu ambapo msimu rasmi ulianza mwezi Juni.

Alisema Mpaka sasa Mapokeo ni Mazuri kwa wananchi mbalimbali kutoka Mikoa ya Mara,Mwanza na Simiyu kitu kinachowapa nguvu ya kuendelea na uzalishaji wa Pamba,chakula cha Mifugo na Mafuta ya kupikia.

 “Kwasasa ndiyo tunaanza Msimu wetu kwa mara ya kwanza maana tunachojivunia mpaka muda huu ni kuwa mapokeo ni mazuri ya wakazi wa mikao ya Simiyu,Mara na Mwanza.”alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kulikuwa na tabu kubwa wakati wa kuanza msimu kwani Wakulima wengi hawakuwa na mtaji hivyo upatikanaji wa Pamba ukawa shida.

Bw Joseph Mathayo ambaye alijivunia ubora wa Mafuta ya kupikia yanayozaliwa na Kiwanda hicho ya nayofahamika kwa jina la Mafuta ya Radha alisema kuwa Mafuta hayo ni meupe ikilinganishwa na Mafuta mengine yaliyopo Sokoni.

 “Mafuta yetu ni Meupe sana na hii inatokana na ubora ambao tunautumia katika kuyatengeneza hivyo ni wananchi kuyajaribu kasha watupe majibu” alisema Bw Joseph Mathayo maarufu kwa jina la Rambo.

Alisema mpaka sasa kiwanda kimeajiri wafanyakazi 55 ambapo uwezo ni kuajiri wafanyakazi 70 huku vibarua wakiwa 120,Bw Mathayo aliongeza kuwa mpaka sasa zipo awamu tatu za kazi na kueleza jinsi wanavyogawa mbegu kwa wakulima na kasha kuwapa madawa.

Akiongelea changamoto zilizopo alisema ni pamoja na Miundombinu iliyopo kwasasa huku changamoto nyingine ilikuwa ni upatikanaji wa vibali wakati kwa kuanza.

Pamoja na changamoto hizo Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wa Mikoa ya Kanda ya ziwa wanaombwa kushirikiana na Kampuni hiyo ili kuendelea kuzalisha lakini kubwa zaidi ni kuendelea kutoa ajira kwa Watanzania.

  “Nadhani kikubwa ni kushirikiana ili kiwanda kiendelee kufanya kazi lakini pia kiendelee kutoa ajira kwa watanzania yaani kama tutazalisha kisha wasituunge mkono tutafunga Kampuni” alisema Mkurugenzi huyo

Kiwanda hicho cha kinamilikiwa na Mfanyabiashara maarufu Mkoani Mara Vedastus Mathayo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa msaada Mkubwa kwa Wakazi wa Mkoa wa Mara na Mikoa Jirani kwa kutoa ajira kwa vijana walio wengi .

No comments:

Post a Comment