Monday, November 19, 2012

RC AAGIZA MAZAO YAFYEKWE ILI KUNUSURU MIGOGORO TARIME *asema mipaka ionyeshwe vizuri *wananchi wataka Serikali kuwekeza eneo hilo

   Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa akisoma ramani na baadhi ya maafisa wilayani Tarime
Na Thomas Dominick,
Tarime.

MKUU wa Mkoa wa Mara John Tuppa ameuagiza  uongozi wa Wilaya ya Tarime  kufyeka mazao yote yaliyomo ndani ya eneo la Serikali  ili kuondo migogoro ya aridhi ya wananchi wa kijiji cha Ng’ereng’ere na kijiji cha Kurutamba.


Agizo hilo limetolewa jana, wakati  alipokuwa katika ziara ya kukagua  eneo hilo  la Serikali  wilayani humo ambalo ndilo linalosababisha machafuko  ya mara kwa mara ya wananchi wa vijiji hivyo viwili.


Tuppa alisema kuwa  mazao  hayo  yaliyomo ndani ya shamba hilo yamekuwa yakisababisha vijiji hivyo  kupigana hasa baada ya kila mwananchi kutakiwa  kuwa katika kijiji chake  kwa kuwa wananchi hao wamekuwa wakilima  shamba hilo kinyume cha sheria.


Pia ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wale wote wanaochochea mapigano kuanzia madiwani ,wazee wa kimila  pamoja na wale wote waliohusika katika mauaji ya mwananchi mmoja hivi karibuni.


Aliwaagiza watendaji wa vijiji  vyote viwili kuhakikisha  wanawajibika ipasavyo ili kuepusha migogoro  ya ardhi katika eneo hilo kwa kuonesha mipaka halali ambayo itasaidia  kila mmoja kuwajibika kulingana na ramani ya mipaka itakayokuwa imeoneshwa.


“Viongozi wa kitongoji na  kata zote ni kwamba wafuate utaratibu tuliopeana tunaomba ufanyike kwani kama ungekuwa umefanyika sisi tusingekuja hapa matatizo hayo tote mngekuwa mmesha yatatua na sio kusubiri mpaka madhara yatokee tumechoshwa na migogoro ya Tarime ya mara kwa mara”Alisema Tuppa.


Alisema  kuwa kitu kikubwa hasa kinachowachanganya wananchi ni mipaka ya kijiji  na mipaka ya eneo lililopo ambalo ndilo linaloleta matatizo  hivyo ambaye hata ridhika   afate utaratibu na sio kuchua sheria mikononi.


Kwa Upande wa wahanga wa mapigano hayo wakazi wa kijiji cha Nyamaraga walisema kuwa  wao wanachotaka ni Serikali kuingilia kati kwa kuwasaidia kutatua matatizo hayo kwani hata wao wamechoshwa na mapigano ya mara kwa mara na wanachokitaka sasa ni maendeleo.


Pia wameiomba serikali kuwekeza kitu chochote katika eneo hilo ambalo ndio chanzo cha migogoro ya mara kwa mara kwa kuwa ni eneo kubwa sana lenye hekta 193.3 na ambalo lipo wazi na lenye rutuba hivyo kufanya wananchi kulima eneo hilo kinyume cha sheria au wapewe sehemu nyingine ili wapate sehemu ya kulima mazao ya chakula.


“Sababu hasa inayosababisha mapigano kati ya vijiji hivi viwili ni oparesheni ya vijiji  ambayo inambidi kila mtu kuwa katika kijiji chake  hii ndio iliyosababisha matabaka ya kila koo kujitenga sasa mazao waliyokuwa wanalina katika shamba hilo nani atayasimamia na ndio yanayoleta migogoro”alisema Christopher Mlimi.


Waliongeza kuwa toka mwaka 1992 eneo hilo ndilo limekuwa chachu ya mapigano baina ya koo mbalimbali katika wilaya hiyo hivyo serikali ichukue hatua za haraka ili kunusuru vifo vanavyotokana na shamba hilo.

No comments:

Post a Comment