Tuesday, November 20, 2012

SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUSAIDIA AKINA MAMA KATIKA KANSA YA MLANGO WA KIZAZI

 Kaimu Mgnaga mkuu wa mkoa wa Mara akipokea vifaa kutoka kwa mkurugenzi wa IMA Bw Jim Cox
 Wanahabari wakiwa busy katika kufanya mahojiano

 Dr Safina Yuma akielezea mpango wa Serikali wa mika Mitano kusaidia akina mama
Serikali imeandaa mpango mkakati wa miaka  mitano utakaowezesha kupamba na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ugonjwa ambao unadaiwa kusababisha vifo vingi vya akina mama nchini.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr Safina  Yuma alisema hayo katika uzinduzi wa huduma za uchunguzi wa Saratani ya Kansa ya Kizazi uliofanyika katika ukumbi wa uwekezaji mkoani Mara.

alisema kuwa huduma hiyo itasaidia kuwagundua akina mama mapema ili wapatiwe huduma kabla madhara hayajawa makubwa na kusababisha kushindwa kutibika.

Dr Yumo Alisema kuwa  tatizo hilo ni kubwa hapa nchini kwa akina mama wengi ambapo wamekuwa na tatizo hilo ambalo lina mahusiano na Hiv.

Aidha  aliongeza kuwa wizara hiyo imekuwa ikitoa miongozo kwa wadau wa afya ambapo kwa sasa imetoa miongozo ya miaka mitano,mbali na hivyo Dr Yuma alisema kuwa huduma hiyo tayari imeishafanyika katika mikoa ya Dar Es Salaam,Morogoro,Iringa,Kilimanjaro,Kigoma,Ruvuma na sasa mkoani Mkoani Mara.

  “Wizara yetu imekuwa ikishirikiana vizuri na wadau mbalimbali na tumekuwa tukitoa Miongozo nah ii itasaidia sana hasa pale wakina mama watakapokuwa wanachunguzwa mapema kabla ya tatizo hilo kuwa kubwa” alisema Dr Yuma

Akizundua Mradi huo unaotekelezwa na shirika la Ima World Health (IMA) yenye muunganiko wa Mashirika manne  yaliyounganishwa na AIDS RELIEF,Kaimu mganga wa mkoa wa Mara Dr Omar Gamoya alisema kuwa ni faraja kwa IMA kuchagua mkoa wa Mara kwani kumekuwepo na ongezeko kubwa la Maambukizi ya ungonjwa wa Ukimwi ambao una Mahusiano na Kansa ya Mlango wa kizazi kwa akina mama.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji  wa Mkoa wa Mara Dr Gamoya alisema mkoa wa Mara upo pembezoni hivyo ni faraja kwa wanaMara kupata huduma hiyo.

    “Tunashukuru sana hawa ndugu zetu kwa kuchagua mkoa wa Mara katika huu mpangango maana Mkoa wetu umekuwa na maambukizi makubwa sana yanyofia asilimi 7.7 na kitaalam kansa hii inaendana na Maambuzi ya HIV” alisema Dr Gamoya.

Dr Gamoya aliongeza kuwa ni vyema wataalam hao wakatumia taaaluma yao vizuri katika kutoa huduma kwa wananchi ambao watakuwa wanasumbuliwa na Matatizo hayo.

Awali akimkaribisha kaimu Mganga Mkuu, Mkurugenzi wa shirika la Kimataifa IMA ambaye pia ni mwakilishi wa Mashirika hayo manne  Bw Jim Cox alisema kuwa Manisapaa ya Musoma itakuwa ni sehemu ya Pili baada ya kuanza na huduma hiyo katika eneo la shirati wilayani Rorya.

Alisema kuwa Tatizo hilo limekuwa likiwapa wakina mama wengi ambapo kati ya akina mama 100 wanaopimwa akina mama saba wanakutwa na tatizo hilo.

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la IMA World Health, Jim Cox alisema kuwa shirika lake kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa ya Aids Relief na Catholic relief Services wameamua kufungua kituo kwaajili ya upimaji wa ugonjwa huo katika hospitali ya serikali ya mkoa wa mara iliyopo mjini musoma.

Pamoja na Uzinduzi huo shirika hilo pia lilitoa vifaa vyenye Thamani ya shilingi Milioni 50 ambavyo vitasaidia katika zoezi la huduma hiyo kwa Manispaa ya Musoma

No comments:

Post a Comment