Jana niliweka habari na Picha za
Anastazia binti anayesumbuliwa na uvimbe wa Mguu wa kushoto ambapo
amekosa fedha za kupata angalau matibabu ya awali,napenda kuchukua
nafasi hii kuwashukuru wale wote walioonyesha kuguswa na habari hii na
mpaka sasa kuna wengine wametuma na wemetoa ahadi ya kutoa fedha za
kumsaidia Anastazia.
Mpaka
sasa Mama Abduweli wa Mamlaka ya banadari Dar es Salaama mwenye namba
0713 689656 ametuma kiasi cha shilingi 10,000 huku dada Edna John kutoka
Uingereza aliyesoma Blog ya Michuzi amesema atatuma fedha za kumsaidia
Anastazia kwenye akaunti.
*Picha
hizo zinaonyesha nikimkabidhi Mama yake na Anastazia
kiasi cha shilingi 10,000 fedha iliyotolewa na mama Abduweli wa Bandari
ya Dar es Salaam,baada ya kukabidhi fedha hizo mama huyo alishukuru na
kusema kuwa itasaidia kupiga Xray kwani hakuwa na kiasi cha shilingi
10,000 kupiga X ray.
Hivyo
basi watanzania tuendelee kumsaidia Annastazia ili aweze kurudi katika
hali yake ya kawaida
aungane na ndugu zake katika ujenzi wa familia yake,kama unamchango
wowote unaweza kupitishia katika akaunti 022201093996 NBC au katika simu
namba 0756 035 825
No comments:
Post a Comment