Wednesday, October 10, 2012

WAWILI WAPOTEZA MAISHA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI MJINI DODOMA

Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon Mdugu mwenye umri wa miaka (70) Mgogo, mkulima na mkazi wa Kisima cha Ndege Mundemu katika wilaya ya Bahi amefariki Dunia baada ya kujeruhiwa na Ndoo Kichwani na katika Taya na mteja wake aliyekuwa akichota maji katika kisima chake.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Stephen alisema tukio hilo lililipotiwa Polisi mnamo tarehe Tarehe 07/ 10/2012 majira ya kumi na mbili jioni (18:00 hrs)  katika kituo cha Polisi Wilaya ya Bahi.

Bw. Zelothe alimtaja mteja huyo ambaye ni  mtuhumiwa katika tukio hilo kuwa ni Bi MAGRETH d/o JOSEPH, mwenywe umri wa Miaka (44) Mgogo, Mkulima ambaye pia ni  mkazi wa Kisima cha Ndege. 

Kamanda Zelothe Stephen alisema chanzo cha tukio hilo ni Ugomvi ulitokea siku ya Jumamosi Tarehe 06/10/2012 Majira ya saa nne asubuhi ambapo Marehemu alikuwa akimdai Bi MAGRETH d/o JOSEPH amlipe pesa Shilingi mia mbili (Tsh 200/=) baada ya kuchota maji katika Kisima chake.
“Bw. Simon Mdugu ambaye ni marehemu  alimtaka Bi Magreth Joseph aliyekuwa amejitwisha ndoo kichwani kumlipa pesa yake, mwanamke huyo alikataa na mara ugomvi ukatokea ndipo akampiga na ndoo hiyo na kumjeruhi Kichwani na katika Taya lake.” Alieleza Bw. Zelothe

Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya  mzee huyo kujeruhiwa alikwenda kupata matibabu katika kituo cha afya cha Mdemu ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, lakini Mnamo Tarehe 07/ 10/2012 majira ya 18:00 kamili jioni alifariki dunia 

Kamanda Zelothe Stephen alisema mtuhumiwa amekamatwa na anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma zinazomkabili.

Wakati huo huo  Gari namba T.624 BAD TOYOTA CRESTA lililokuwa likiendeshwa na Jasiri Maligo, Miaka (44), Mbena, mkazi wa Ipagara lilimgonga mtembea kwa miguu ambaye hakufahamika jina, mwanaume, umri kati  ya miaka 35-40 na kumsababishia kifo.

Kamanda Zelothe alisema tukio hilo lilitokea tarehe 07/10/2012 majira ya saa tatu usiku, katika eneo la Chaduru kata ya Makole tarafa ya Mjini katika Manispaa ya Dodoma kwenye barabara kuu ya DODOMA/MOROGORO.

Akizungmzia Chanzo cha Ajali hiyo, alisema kuwa ni uzembe wa Dereva, aidha alisema Dereva wa gari hiyo amekamatwa na atapelekwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment