Friday, October 12, 2012

MRADI MKUBWA WA MAJI MAJI KUANZA KUTEKELEZWA MUSOMA MJINI


-Pia watumishi wa idara ya maji Mugango,Kiabakari na Butiama wafikisha madai ya mishahara ya miezi 26 hadi miaka mitatu

-Pia hakuna mwandishi aliyeshushwa na Muwasa kushiriki katika ziara ya naibu waziri kama ilivyoripotiwa awali

HATIMAYE Serikali imepanga kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara ambao unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 41.

Naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Benilith Mahenge,ametoa taarifa hiyo mjini Musoma wakati akizungumza na uongozi wa mkoa wa Mara,ambapo amesema tayari mipango wa kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa imekamilika baada ya serikali kupata fedha kutoka nchi za Ujerumani na Ufaransa.
Amesema mradi huo pamoja na kuchelewa kuanza utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka mitatu lakini utalenga kuhamisha chanzo cha maji cha sasa na kujengwa upya katika eneo la Bukanga pamoja na kufufua na kuongeza miundombinu  mipya ya maji ili kukidhi hitaji  la maji kwa wananchi na taasisi zote katika Manispaa ya Musoma.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tupa,pamoja na kupongeza hatua hiyo ya serikali kwa kukubali kutekeleza mradi huo katika unaolenga kuwandolea kero kubwa ya upungufu wa maji inayowakabili wananchi lakini pia ameahidi kuwa serikali ya mkoa itahakikisha inapambana na vitendo vyote vya hujuma ambayo inaweza kujitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.

Wakati huo huo baadhi ya watumishi wa serikali katika mradi wa maji wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama wanadai mishahara yao ya kati ya miezi 26 hadi 30 jambo ambalo limewafanya kuishi maisha ya kuomba omba.

Wafanyakazi hao wametoa kilio hicho baada ya naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Binilith Mahenge kutembelea mradi huo ambao pia umekuwa ukikabiliwa na uchakavu mkubwa wa miundombinu ya kusambazia maji kenda kwa wananchi ikiwemo familia ya baba wa Taifa hayati Mwl Julius Nyerere.

Wakiwa na mabango wafanyakazi hao ambao wengi ni vibarua wa kudumu wamemueleza na naibu waziri huyo kwa nyakati tofauti kuwa  hivi sasa baada ya kutoka kazini wanalazimika kufanya vibarua vikiwemo vya kulima mashamba kwaajili ya kupata fedha za kuhudumia familia zao.

Kufuatia kilio hicho,naibu waziri huyo wa maji,ameuagiza uongozi wa mamlaka ya maji ya Mugango,Kibakari hadi Butiama,halmashauri ya Musoma na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Butiama kumpatia maelezo ya sababu za wafanyakazi hao kutolipwa mishahara yao kwa kipindi hicho pamoja na kuorodhesha madai yote ambayo yanadaiwa na watumishi hao ndani ya siku tatu.

Amesema kushindwa kulipa mishahara hiyo kwa wakati kunaweza kuchangia watumishi wasio waaminifu kufanya hujuma kubwa ikiwa ni pamoja na kuiba mashine za mradi huo jambo ambalo linaweza kuingizia hasara kubwa serikali huku  akitoa mwezi mmoja kwa meneja wa mradi huo mhandisi Merchedes Tibita kuongeza ukusanyaji wa mapato ambayo yatawezesha kutatua baadhi ya changamoto zinazoukabili mradi huo.

KUMRADHI


katika habari aambayo imewekwa humu ambayo ilikuwa ikisema kuwa waandishi wa habari wameshushwa ndani ya gari na kumnukuu Afisa Mawasiliano  Mamlaka hiyo si  Sahihi,Taarifa sahihi ni kwamba Mamlaka hiyo iliwaalika waandishi ambao wapo ndani ya uwezo wao na kuamua kuchukua vyombo vinne ambavyo ni ITV,CHANNEL TEN,TBC na Gazeti la CITIZEN hivyo waandishi ambao walilalamika kuwa wameshuhswa hawakuwa na mwaliko kutoka katika Mamlaka hiyo

Hivyo mtandao huu ambao pia ulirusha habari hiyo unaomba radhi kwa Mamlaka hiyo kwa usumbufu uliojitokeza na ziara ya Naibu waziri bado inaendelea na leo wapo katika wilaya ya Serengeti. 

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI MH ENG DK BINILITH MAHENGE WILAYA ZA MUSOMA NA BUTIAMA

 Naibu waziri wa Maji Mh Dk Binilith Mahenge akiwa pamoja na DC Musoma Jackison Msome na mkurugenzi wa MUWASA Gines Kaduei
 Mh Mahenge akiwa pamoja na viongozi wa wilaya ya Butiama
 Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura wa kwanza kulia akiwa na naibu waziri wa maji na viongozi wa Manispaa ya Musoma
 Picha ya juu mkurugenzi wa Muwasa akimunyesha mitambo naibu waziri wa maji
 Chanzo cha maji cha Muwasa katika ziwa victoria ambacho kinahitajika kuhamishwa kwa gharama ya bilioni 41 kwaajili ya kuwezesha mji wa Musoma kupata maji ya uhakika
 Sehemu ya mji wa Butiama
 Viongozi wa wilaya ya Butiama wakiwa na naibu waziri wa maji wa kwanza kushoto ni Magina Magesa m/kiti wa halmashauri ya Musoma
 Chanzo cha maji cha mradi wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama
 Naibu waziri akiwa pamoja viongozi wa wilaya ya Butiama
 Bango la wafanyakazi wa maji Mugango/Butiama ambao wanaidai serikali miezi 26 hadi miaka mitatu
 Sehemu ya mji wa Butiama

 Naibu waziri wa maji Mh Mahenge akisoma moja ya bango
 Naibu waziri wa maji akiangalia Bwawa la Kiarano


 Naibu waziri akitoa heshima katika kaburi la Baba wa taifa kijijini Butiama

 Emanuel Ams wa TBC akisalimiana na mjane wa baba wa Taifa mama Maria Nyerere
 Naibu waziri akisalimiana na mama Maria Nyerere
 Naibu waziri akitoa neno la shukurani kwa Mama Maria Nyerere

No comments:

Post a Comment