WANAWAKE wanaojishusha hadhi kwa kujirahisisha katika Nyanja mbalimbali katika jamii ikiwemo burudani biashara na katika siasa wametakiwa kuacha tabia hiyo mara moja kwa kuwa siyo desturi kwa mwanamke kujihusisha na mambo hayo kwani yanapoteza fursa na haki zao katika jamii.
Hayo yamesemwa na Ritha Mlagala
makamu mwenyekiti wilaya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini
katika
mdahalo wa haki na fursa sawa kwa jinsia zote uliofanyika katika kata ya
Nzihi jimbo la Kalenga Iringa ulioandaliwa na mtandao wa
mashirika yasiyo ya kiserikali katika mkoa wa Iringa (ICISO-UMBRELLA).
“Ipo dhana potofu ambayo
imejengeka miongoni mwa wanawake wengi kuwa wanaume ndio wenye maamuzi makubwa
katika na kumpa madaraka makubwa katika kufanya maamuzi na hivyo kuwafanya
wengi kukubali kutumiwa katika vitu vingi vya starehe mfano kutumiwa katika
nyimbo za wasanii na katika siasa kufanya kampeni kwa wengine huku wakiziacha nafasi hizo kwa
kudhani kuwa hawana uwezo wa kuongoza”alisema Mlagala
Ameeleza kuwa ipo haja kubwa ya
wanawake kusimama na kujua haki zao katika Nyanja za kimaendeleo katika jamii
kama siasa. Na kusema serikali imetoa fursa nyingi sana kwa wanawake lakini
wameshindwa kuzitumia na kuwataja baadhi
ya wanawake ambao wamefanikiwa katika siasa akiwemo yeye pamoja na wenye
msimamo kama Dkt Asha Rose Migiro ambao wana nafasi kubwa katika siasa kwa sasa.
Pia ameongeza kuwa wanawake wengi
wamekuwa hawana upendo na wamekuwa wakikatishwa tama na wanawake wenyewe kwa
kudharauliana kuwa hawawezi na kuwataka wanawake kujiheshimu na kuvaa mavazi
yanayositiri miili yao ili kuweza kuboresha maadili katika jamii.
Maria sanga ni mama mkazi wa
kijiji cha Nzihi anakiri kuwa wanawake wengi hawajaelimika na hawajiamini na hii
ni kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kuhusu haki zao.
“Tatizo kubwa kubwa sisi wakinamama
sisi wenyewe kwa wenyewe hatuaminiani lakini kama elimu hii ya fursa na haki itaendelea
kumuelimisha huyu mwanamke kweli tunaweza kuelimika mwanamke akielimika jamii
nzima itaelimika”alisema sanga
Naye Abdusalani Mkata ameilaumu serikali
na ngazi za juu katika unyanyasaji wa mwanamke na kueleza kuwa wanawake wengi
wamekuwa wakoneshwa maungo yao katika televisheni na katika mabango ya
matangazo na serikali bado inafumbia macho hali hiyo na kutoipiga marufuku na
kufanya tabia hiyo kuonekana ya kawaida na kuendelezwa katika jamii.
James Ndota ameeleza kuwa
amegndua wanawake wengi hawapati haki zao hii ni kutokana na wao wenyewe
kutoamini kuwa fursa wanaopewa kuwa wanaweza na kutoa mfano wa vikundi
mbalimbali vilivyopo katika jamii wanaposhirikishwa katika vikundi
vinavyojumuisha wanaume na wanawake wengi wao hukwepa na kusema kuwa hawawezi
na kuwa wamekuwa hawajiamini.
==================================
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mhe.Ritta kabati ametoa mifuko kumi ya
saruji ,madawati na vitabu kwa shule ya msingi kibwabwa wakati wa
mahafari ya shule hiyo yaliyofanyika leo katika viwanja vya shule
sekondari ya hiyo kata ya kitwiru mkoani Iringa .
akizungumza na
wazazi na wanafunzi wa shule hiyo katika mahafari hayo amesema kwamba
wazazi wanatakiwa kuchangia zaidi katika elimu ya msingi kwa kuwa ina
matatizo makubwa sana na elimu ya msingi ndio kila kitu hivyo hakuna
budi wazazi wawape msingi mzuri wa elimu kuliko kuchangia zaidi katika
mambo ya sherehe.
shule hiyo inakabiliwa na matazizo ya
vyoo, vitabu na madawati na viwanja vya michezo na kwa kuelewa hivyo
mbunge huyo wa viti maalimu ametoa vitu hivyo kwa lengo la kujengea
choo cha walimu ambako hapo mwanzo walimu wanachangia choo na wanafunzi.
aidha amewapongeza wazazi na walimu wa
shule hiyo kwa juhudi kubwa wanayofanya kupandisha kiwango cha elimu
katika shule hiyo kuliko ilivyokuwa mwanzo.
No comments:
Post a Comment