Monday, October 15, 2012

HIVI NDINYO MVUA ILIVYOHARIBU MAKAZI YA KAYA 21 KATA YA BWERI MANISPAA YA MUSOMA

MEYA WA MANISPAA YA MUSOMA ALEX KISULULA AKIANGALIA BAADHI YA NYUMBA ZILIZOHARIBIWA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MKOANI MARA NA MAENEO MENGINE YA NCHI

WAKAZI WA MTAA WA BUKOBA KATIKA KATA YA BWERI AMBAO HAWANA MAKAZI KUTOKANA NA NYUMBA ZAO KUEZULIWA NA UPEPO ULIOAMBATANA NA MVUA KUMBWA

MMOJA WA WAKAZI WALIATHIRIKA NIKIMCHUKUA MAELEZO

MEYA NAE ALITOA TAHADHARI YA KUHAMA MABONDENI KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Na Shomari Binda,
Musoma

JUMLA ya kaya 21, Kata ya Bweri, Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara zimekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka kutokana na upepo mkali na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha Oktoba 11 mwaka huu.

Waandishi wa habari wakiwa na Meya wa Manispaa hiyo Alex Kisururawalifika katika eneo lilioharibiwa ambapo ilishuhudia wakazi wa nyumba hizo wakiwa nje ya nyumba zao huku wengine wakifanya juhudi ya kukarabati ili kuweza kujisitiri.

Baada ya kufika eneo hilo baadhi ya wananchi walisema kuwa mvua hiyo kabla ya kunyesha ulianza upepo mkali pamoja na vumbi kama moshi kasha mvua kubwa iliyoambatana na mawe.

“Kwanza ulianza upepo mkali ulioambatana na vumbi kubwa kama moshi kasha ilikuja mvua kubwa iliyonyesha kama saa moja hivi ambapo ilisababisha nyumba zetu nyingi kuezuliwa na nyingine kuanguka kama unavyoona,”alisema Matiku Zakaria.

Baada ya mvua hiyo kuisha mali za wakazi hao hazikujulikana dhamani yake zilikuwa zimeharibiwa vibaya ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa kuwa mvua hiyo ilinyesha jioni.

Wakazi walifikwa na maafa hayo ni Matiku Kitogoro, Zakaria Kitogoro, Manyonyi Kitogoro, Fredrick Ibaso, Albinus Ogono, Kibaso Itinde, Itende Warioba na Mwalimu Kanoga.

Wengine ni Nyamamba matiku, Joseph Magoti, Ghati Regu, William Julius, Wambura Itinde, Mashaka Mbeshi, Nyamoko Magoti na Bahati Itinde na nyumba zingine tano zilizokuwepo katika  mtaa wa Rwamlimi katika katahiyo.

Diwani wa kata hiyo Shaban Sondobi alisema kuwa baada ya maafa hayo alipigiwa simu na kwenda kuona uharibifu huo sambamba na kumtaarifu meya wa manispaa hiyo.

Naye Meya Kisurura amewaagiza watendaji wa kata hiyo kuwapatia Elimu juu ya ujenzi salama wa nyumba hasa kipindi hiki ambapo watabiri wa hali ya hewa wametoa taarifa kuwa nchi nzima itakuwa na mvua kubwa.

“Watendaji ebu anzeni kutoa Elimu kwa wakazi wenu kabla hawajaanza kujenga na hata hivyo nyumba nyingi tulizotembelea zimechoka sana lakin pia jitahidini kutoa habari mapema mamlaka husika panapotokea maafa kama haya.

Kisurura amesema kuwa taarifa tayari imefika katika kamati ya maafa ya manispaa hiyo ili kufanya tathimini ili kuweza kuwasaidia wakazi hao lakini pia ametoa rai kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama kabla hawajafikiwa na maafa ya mafuriko.


chanzo Shom B

No comments:

Post a Comment