MUSOMA.
MAMLAKA ya Majisafi na taka Manispaa ya Musoma mkoani
wa Mara (MUWASA) imewashusha waandisha wa habari njiani waliokuwa katika ziara
ya Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Dk.Eng.Binilith Mahenge kwa madai
ya kisingizio cha ufinyo wa bajeti.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa magezeti ya mbalimbali
mkoani hapa wameshushwa katika eneo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Manispaa ya
Musoma na Afisa Mahusiano wa Mamlaka hiyo Emmanuel Ruyobya hali ambayo ni imeonekana kuwa ni udhalilishaji.
“Kiukweli huu
ni udhalilishaji kwani sisi tuna vyombo vyetu ambavyo tunavifanyia kazi na si
lazima tulipwe posho sasa huyu yeye anasema bajeti finyu wakati sisi hatujaomba
posho” alisema mmoja wa waandishi wa habari walioshushwa katika gari hiyo.
Akisoma taarifa
ya Maendeleo na Changamoto zake katika ofisi ya mkuu wa mkoa kwa Naibu,Katibu
Tawala wa mkoa hupo Climent Lujaji alimuagiza mkurugenzi wa MUWASA Genes Kaduri
kuwaweza waandishi hao katika suala la usafiri ili waweze kushiriki katika
ziara hiyo ambapo mkurugenzi huyo alimkubalia .
Aidha Baada ya kuondoka katika eneo la ofisi wa mkoa
waandishi wa habari hao walishishwa katika gari hiyo kwa madai hayo na kwamba
wameishaalika waandishi wao .
“Kama Katibu Tawala wa mkoa ndiye kawaambia muje nendeni
awalipe na kuwatafutia usafiri.,alisema Afisa mahusiano Ruyobya kwa jaziba kubwa.
Tabia ya kuwashusha waandishi wa habari si la mara ya kwanza katika ziara mbalimbali
zinazofanywa na viongozi kama hao mkoani hapa hususani katika vyombo habari vya magazeti kubaguliwa na hata hivi karibuni 5 Oktoba mwaka huu imefanyika ziara ya Naibu waziri wa Nishati
na Madini Stephen Masele ambapo pia
vyombo vingine vimebaguliwa.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Binilith Mahenge ameaza ziara yake ya kujua maendeleo na
changamoto zake mkoa wa Mara ambapo imeanzia katika halmashauri ya wilaya
ya Manispaa ya Musoma,Butiama kukagua
chanzo cha maji cha Mugango –Kiabakari, Rorya,Serengeti na kumalizia
wilaya ya Bunda.
No comments:
Post a Comment