Dinna Maningo,TARIME,
Mwenyekiti
wa kijiji cha Nyamwaga Wilayani Tarime Sasi Kirigiti (CCM) ameuomba Mgodi wa Africa Barrick Gold Mine kutoa taarifa za gharama za fedha zinazokuwa zimetumika kutekeleza miradi yao
pindi wanapoikabidhi kwa wananchi kama njia ya kupunguza malalamiko yanayojitokeza
juu ya kutotolewa kwa taarifa ya fedha katika miradi ya mgodi.
Kirigiti
amesema kuwa Mgodi unapaswa kufika sehemu
kuwa wawazi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za fedha zinazotumika kwenye miradi yao kupitia maandishi nasiyo kusema kwa mdomo
ili iweze kutunzwa kama kumbukumbu
na uongozi wa Serikali ya kijiji na kwamba siyo sahihi taarifa za fedha
kutolewa ndani ya mgodi na badala yake
fedha hizo zisemwe moja kwa moja mbele ya wananchi na viongozi wa
serikali ya kijiji ili wajiridhishe.
Hayo
ameyasema jana wakati Naibu Waziri wa mazingira Charles Katwanga
akikabidhi kisima cha maji kwwa wananchi wa kijiji cha Nyansangero
kilichochimbwa kwa msaada wa mgodi wa North Mara ABG wakati
wakiwa kwenye Ziara yao mgodini akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa
Madini Stivin Masele na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mkuu wa
shule ya Msingi Nyansangero Wambura
Mwita amesema kuwa msaada huo wa kisima
utawasaidia wananchi pamoja na
shule hiyo kuondokana na tatizo la maji ambalo limesumbua kwa muda mlefu ambapo pia
aliutaka mgodi kutoa taarifa ya fedha za miradi wanapoikabidhi kwa wananchi kwa madai kuwa mgodi ulijenga
tenki la maji shule ya msingi Nyansangero pamoja na maasa wa
madawati 91 lakini hawakuwafahamisha
wala kubainisha gaharama
zilizotumika kujenga tenki pamoja na
gahara za kila dawati.
MANAIBU WAZIRI WALALAMIKIWA KUKABIDHI KISIMA BILA KTAJA
GHARAMA
Dinna
Maningo,Tarime.
BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Nyansangero Kata ya
Nyamwaga Wilayani Tarime wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Naibu Waziri wa mazingira
Charles Kitwanga na Naibu Waziri wa madini Stiven Masele kukabidhi kisima cha
maji kwa wananchi kilichojengwa kwa
msaada wa Mgodi wa Afica Barrick Gold MineABG wa Nyamongo bila kuwajulisha
kiasi cha fedha zilizotumika kukamilisha ujenzi wa kisima.
Kisima hicho kilichimbwa kwa msaada wa mgodi na kukabindiwa jana kwa wananchi na Naibu Waziri wa mazingira Charles Kitwanga wakati
wakiwa kwenye Ziara yao katika mgodi
wa North Mara ABG, ambapo wananchi
waliukuwepo kwenye makabidhiano walisema hawafahamu kimechimbwa na kukamilika
kwa kiasi cha shilingi ngapi jambo ambalo limezua malalamiko kwa wananchi wa
Nyansangero.
“Nimesikitika kuona Waziri Kitwanga akikabidhi kisima kwa wananchi bila hata sisi kujua ni kiasi gani cha pesa kimetumika katika
ujenzi wa kisima mimi nilitarajia kabla Waziri ajakata utepe angeuliza mgodi fedha zilizotumika
badala yake akaa kimya na hata Waziri Masele naye alikaa kimya bila hata kuhoji sanjari na
viongozi wa Wilaya,wanakabidhi kisima kiholela hawajasema kina urefu wa futi ngapi
kwani hadi wanaotoka eneo la tukio mgodi
haukusema kiasi cha pesa kilichotumika”alisema Chacha Mwita.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Nyamwaga Wilayani Tarime Sasi Kirigiti (CCM) ameuomba Mgodi wa Africa Barrick Gold Mine kutoa taarifa za gharama za fedha zinazokuwa zimetumika kutekeleza miradi yao
pindi wanapoikabidhi kwa wananchi kama njia ya kupunguza malalamiko yanayojitokeza
juu ya kutotolewa kwa taarifa ya fedha katika miradi ya mgodi.
“Naupongeza
mgodi kwa msaada wao wa kuchimba kisima
cha maji kitasaidia wananchi
kuondokana na tatizo la maji lakini naushauri mgodi unapokabidhi miradi
yao watoe taarifa ya moja kwa moja kwa wananchi juu ya kiasi
cha pesa kilichotumika kwenye miradi yao wanapoondoka bila kusema wanazua malalamiko
kwa wananchi ambao walitaka kufahamu pesa zilizotumika ,pia watoe taarifa
mapema ili wananchi waalikwe kuhudhuria
kwenye miradi .”alisema Kirigiti
Kirigiti
alisema kuwa Mgodi unapaswa kufika sehemu
kuwa wawazi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za fedha zinazotumika kwenye miradi yao kupitia maandishi nasiyo kusema kwa mdomo
ili iweze kutunzwa kama kumbukumbu
na uongozi wa Serikali ya kijiji na kwamba siyo sahihi taarifa za fedha
kutolewa ndani ya mgodi na badala yake
fedha hizo zisemwe moja kwa moja mbele ya wananchi na viongozi wa
serikali ya kijiji ili wajiridhishe.
Mkuu wa
shule ya Msingi Nyansangero Wambura
Mwita alisema kuwa msaada huo wa kisima
utawasaidia wananchi pamoja na
shule hiyo kuondokana na tatizo la maji ambalo limesumbua kwa muda mlefu ambapo pia
aliutaka mgodi kutoa taarifa ya fedha za miradi wanapoikabidhi kwa wananchi kwa madai kuwa mgodi ulijenga
tenki la maji shule ya msingi Nyansangero pamoja na maasa wa
madawati 91 lakini hawakuwafahamisha
wala kubainisha gaharama
zilizotumika kujenga tenki pamoja na
gahara za kila dawati.
No comments:
Post a Comment