Sunday, October 7, 2012

IGP ATAKA KILA MWANANCHI KUWA MLINZI WA TAIFA LETU


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

ZANZIBAR JUMAMOSI OKTOBA 6, 2012. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa ili kuifanya nchi yetu iendelee kuwa salama, kuna haja ya kuwekeza zaidi katika miundombinu ya amani.

IGP Mwema ameyasama hayo leo mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi wa kati kwa askari Polisi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi mjini Zanzibar.

Amesema bado kuna haja ya kila mwananchi kuelewa kuwa jukumu la usalama wa nchi hii liko mikononi mwake.

Amesema kila mmoja hawezi kukwepa jukumu la kulinda rasilimali yake na mfano mdogo ni pale kila mmoja kwa wakati wake na bila ya kufundishwa pale anapolinda faragha.

IGP Mwema pia ameeleza umuhimu wa kwa nini kila Mtanzania anapaswa kuwa  mlinzi wa Taifa letu na kutilia mfano kwamba suala la ufalama linaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, kaya, kijiji, kata ama shehiya tarafa wilaya mkoa na Taifa.

Amesema katika taaluma ya Polisi, Askari amefundishwa kuwa mlinzi katika mambo manne makubwa ambayo yanamhusi kila mmoja wetu bila ya kujali nafasi yake katika jamii.

Mambo hayo ni manne ni fursa ambazo zikiachwa wazi watu wengine wanachukua nafasi ya kuichukua nafasi kuu nne ( four Speces )  sio  kama askari lakini hatani  kabla ya wa mali wa mali zake, mlinzi wa familia wakiwemo watoto wake pamoja na himaya inayomzunguuka.

Amewataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake, awe mdau wa sualama kama anavyolinda na kuheshimu faragha zake.

Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuna haja ya kila kiongozi wa Jeshi la Polisi hapa nchini kuyageuza matazo wanayowakabili kama changamoto na kuzigeuza fursa ya kuleta ufanisi kazini.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi, ameelezea mikakati inayochukuliwa na mkoa wake katika kudhibiti usalama wa maeneo mbalimbali na kusema kuwa Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ni jicho la Polisi mitaani.

Awali akitoa tathmini ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Zanzibat ACP Ramadhani Mungi, amesema wahitimu hao wamejifunza mambo mbalimbali ukiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi na vyombo vya Habari.

Kamanda Mungi, amesema wameweka somo hilo kwa kufahamu kuwa kazi za Polisi zinaingiliana kwa kiasi kikubwa na zile za Waandishi wa Habari na kwamba kila mmoja anamtegemea mwingine ili kufanikisha kazi zake.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Kamishna Khalifa Hassan Choum, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Dar es Salaam ACP Ali Lugendo na Maafisa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vikosi vya SMZ

No comments:

Post a Comment