Tuesday, October 2, 2012

IGP SAIDI MWEMA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO ZANZIBAR


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

ZANZIBAR JUMANNE OKTOBA 2, 2012. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Ijumaa na Jumamosi wiki hii, atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo ya uongozi mdogo kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi Zanzibar.

Taarifa ya Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar (Zanzibar Police Academy) SSP Raamadhani Mungi, imesema kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yatafungwa katika awamu mbili tofauti.

Amesema awamu ya kwanza, mafunzo hayo itafanyika katika chuo cha Mafaafisa wa Mafunzo (Magereza) kilichopo eneo la Hanyengwa mkoa wa Kusini Unguja ambapo yatafanyika maonyesho ya utayari na Medani za kivita.



Kamanda Mungi amesema maonyesho hayo yatanza saa 9.00 Arasili siku ya Ijumaa Oktoba 5, mwaka huu, kwa kuwashirikisha Wahitimu wa vyeo vya RSM na Staf  Sajent waliokuwa wakishiriki katika mafunzo hayo.

Amesema sherehe hizo zitafuatiwa na zile zitakazofanyika kwenye Viwanja vya Polisi Ziwani mjini Mjini Zanzibar zitakazoanza saa 2.30 asubuhi siku ya Jumamoori Oktoba 6, 2012.

Kamanda Mungi amesema siku hiyo asubuhi, IGP Mwema, atakagua gwaride kabla ya gwaride hilo kupita mbele yake kwa mwendo wa pole na mwendo wa waharaka kwa heshma.

Kamanda Mungi ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vya Jendele, Ndigani, Cheju, Kwaka, Tunguu, Dunga na wenyeji Hanyegwa pamoja na wakazi wa mjini Zanzibara na Viunga vyake, kufika kwa wingi katika Chuo hicho cha Hanyegwa na Ziwani ili kujionea maonyesho mbalimbali.

Zaidi ya Askari 920 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya Sajenti, Staf Sajent na RSM watahitimu mafunzo yao na kutunukiwa vyeo vipya.

No comments:

Post a Comment