Monday, October 1, 2012

KIKUNDI CHA ELIMIKA CHAJIVUNIA RUZUKU YA FFCS


Kikundi cha Elimika Musoma mjini kimeishukuru Taasisi ya The Foundation for Civil Society ya jijini Dar Es Salaama kwa ufadhili walioutoa kwa kikundi hicho katika Kujijengea Uwezo.

Akiongea ofisini kwake Mratibu wa Kikundi hicho Bi Dora Maro alisema kuwa Taasisi hiyo ya The Foundation for Civil Society ilitoa ufadhili wa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni Saba katika mradi wa kujijengea uwezo kwa mwaka 2010/2011 ambapo mradi huo ulikuwa ukitekelezwa katika Kata za Bweri,Nyakato na Nyasho

  Baadhi ya Taarifa za kikundi hicho nikizizoma kwa umakini mkubwa

Amesema katika kutekeleza mradi huo kikundi hicho kimepata faida kubwa kutokana na Viongozi na Wanachama wake  kujua hali halisi ya uongozi,mapungufu yaliyopo katika Kikundi chao na kuyafanyia kazi.

Bi Dora alisema kuwa Kumekuepo na mabadiliko makubwa katika Jamii tangu wamepewa ufadhili huo ambapo alisema kuwa wameweza kujua jinsi ya Kupanga Miradi ya Kibiashara na kuendesha biashara hizo.

Alisema mbali na hivyo wamejua pia kupanga miapango mikakati na mipang kazi,kuwa wabunifu wa miradi,ufuatiliaji na usimamizi wa fedha pamoja na utunzaji wa kumbukumbu.

Akiendelea kueleza faida walizozipata kutokana na Mradi huo waliokuwa wakiuetekeleza kupitia ruzuku kutoka The Foundation for Civil Society,Bi Dora alisema kuwa pia Mradi huo umesaidia kubadilisha Mtazamo katika jinsi ambapo baadhi ya watu wameendelea kusema Mwanamke hawezi hivyo Mradi huo umesaidia kuleta mabadiliko ya Kifikra katika Jamii.

Katika kukamilisha Mradi huo Mratibu wa Kikundi hicho alisema kuwa wameweza kuwashirikisha watu mbalimbali katika kujengewa uwezo ikiwa njia ya kuendesha Maisha yao,baadhi ya watu walioshirikishwa katika Mradi huo ni pamoja na Waathirika wa Ugonjwa wa Ukimwi,Wajane na Walemavu

 “Sisi tuliamua kuwashirikisha hawa wenzetu kwasababu tuliona kuwa wanasahaulika na pia  tulifanya hivyo ikiwa ni njia ya kuwasaidia kuendesha Maisha yao baada ya huu Mradi” alisema Bi Dora

Kuhusu  Ushirikishwaji wa Jamii katika Mradi huo Bi Dora alisema kuwa walifanikiwa katika hilo kwani Viongozi waliowahitaji kushirikiana nao walijitokeza na hivyo kuwasaidia katika kuhamasisha Jamii katika kukiunga Mkono Kikundi hicho.

Bi Dora alisema kuwa kulikuwepo na hamasa kubwa kwa Wananchi ambao Mradi huo ulikuwa umehusisha baadhi ya watu ikiwa ni njia ya kuwajengea Uwezo wa Kimaisha,huku akisema kuwa wamefikia Malengo yao ya Sera ya Ushirikishwaji katika Jamii kutoka katika Kikundi hicho.
Pamoja na kupata ruzuku kutoka The Foundation for Civil Society ya jijini Dar Es Salaam,Mratibu huyo alisema kuwa kikundi chake kina Mahusiano Mazuri na baadhi ya Makampuni na wafadhili kutoka ndani mfano akiongelea Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) ambapo umewahi kuwasaidia.

Pamoja na kutekeleza Mradi huo kwa kiwango kikubwa Bi Dora alisema kuwa kulikuwepo na changamoto mbalimbali katik kutekeleza Mradi huo ikiwemo wanachama kuwa na uelewa mdogo juu ya ruzuku hiyo,kutokujua nini maana ya Mpango mkakati na mpango kazi,Utunzaji wa Fedha na wananchi kudhani kuwa ruzuku hiyo ni ya kutumia katika kuendesha Maisha yao.

                   Baadhi ya wanakikundi

Wakiongelea kuhusu Mradi huo baadhi ya wanachama walionufaika na Mradi huo ni pamoja na Bi Judith Semen ambaye alisema kuwa amenufaika kwa kiasi kikubwa na mradi huo kutokana na kuelewa mambo mengi yanayohusiana na utunzaji wa Fedha.
 “Mimi nilikuwa sijui jinsi ya kutunza fedha kitaalamu lakini baada ya mradi huu wa kutujengea uwe nimeweza kujua na nafurahi maana hata nikiamua kufungua biashara naweza kufanya vizuri” alisema Bi Judith

Naye Jenipher Danga,Halima Mohamed na Debora Kopoka walisema kuwa wamenufaika kwa kiasi kikubwa kwani ni mambo mengi ambayo wamejifunza kutoka katika Mradi huo na hivyo kuwa kuna haja ya kuendesha mambo kitaalamu na si kimazoea.

Katika upande wa Serikali kushirikishwa katika Mradi huo,Mtendaji wa Kata ya Bweri Bw. Jamhuri Makongoro alisema kuwa Kikundi hicho cha Elimika Musoma mjini kimeweza kushirikiana vyema na Serikali ya mtaa huo lakini pia kimesaidia wanawake wengi ambao ni Wajane,waathirika na Walemavu katika kuwajengea Uwezo wa kimaisha.

 “Nashukuru Kikundi hiki kimeweza kushirikiana na Serikali ya mtaa vyema na hasa kimesaidia sana Wajane,Walemavu na watu walioathirika na ugonjwa wa Ukimwi” alisema Mtendaji huyo.

Aidha akiongelea Faida ilizozipata kikundi hicho kutokana na ufadhili wa The Foundation For Civil Society,Bi Dora alisema kuwa kupata ruzuku hiyo imewasaidia kupata mafunzo ambayo yamesaidia kuendesha Kikundi hicho kwa ufanisi mkubwa,kuimarika katika kubuni Miradi na kuiendesha,matumizi sahihi ya Fedha,kusaidia Jamii ambayo ilihitaji msaada wa kuwajenga kiuwezo,utunzaji wa kumbukumbu,kupanga Mipango mikakati na Mipango kazi,ufuatiliaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali na kujua udhaifu wa Kikundi hicho

Mbali na hivyo Bi Dora alisema kuwa kupata ruzuku kutoka katika Taasisi hiyo imesaidia kuaminika kwa Asasi hiyo mbele ya Jamii na Viongozi wa serikali kitu ambacho aliishukuru sana taasisi ya The Foundation for Civil Society.

“ Kiukweli hii Taasisi imetupatia sana heshima kwa kutupatia ruzuku maana tunaaminika kwa Jamii na hata kwa Viongozi wa Serikali kitu ambacho ni lazima tuishukuru The Foundation for Civil Society” alisema Bi Dora

No comments:

Post a Comment