SERIKALI
imeunga mkono wazo la waziri mkuu mstaafu Edaward Lowassa kwa kukiri kuwa
endapo hakutakuwa na mkakati thabiti wa kushughulikia tatizo la ajira kwa kundi
la vijana kuna hatari kubwa ya kuleta machafuko katika siku za usoni.
Kauli hiyo
ilitolewa na juzi wilayani Meatu na waziri wa nchi ofisi ya Rais Muhusiano na
Uratibu Stephen Wassira wakati akizungumza na viongozi wa wilaya hiyo ikiwa ni
siku ya pili ya ziara yake mkoani Simiyu.
Kauli ya waziri
Wassira imekuja kukiwa na kauli kadhaa ambazo zimekuwa zikitolewa na waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa Munduli Edaward Lowassa kuwa tatizo la ajira kwa
vijana ni sawa na bomu.
Akizingumza
na viongozi wa Meatu mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wakiongozwa na mwenyekiti
wake Rossemary Kirigini,Wassira alisema kuwa tatizo la ajira kwa kundi la
vijana ni kubwa sana na kwamba linatishia amani hivi sasa.
“Asilimia 60
ya watanzania ni vijana na hawana ajira hivi unategemea nini ndio maana
wakiambiwa kuna maandamano wao hawaulizi maandamano hayo ni ya nini
wanachouliza yananzia wapi na kwenpi tu”alisema na kuongeza.
“Hatuwezi
kuwa taifa huku kundi kubwa la watu ambao ni vijana halina kazi hivyo kama
viongozi lazima sasa tuchukue hatua mbalimbali kwa kutumia fursa tulizo nazo
ili tuhakikishe tunapambana na changamoto hii”alisema Wassira.
Kwa sababu
hiyo alitaka kupitia Tasaf awamu ya tatu pamoja na kulenga kuwezesha familia
masikini kwaajili ya kuwangezea kipato ili kupambana na umasikini lakini pia
halmashauri nchini kote zihakikishe zinahamasisha uundwaji wa vikundi vya
vijana vya uzalishaji mali ambavyo vitawezeshwa ikiwa ni njia moja wapo ya
kukabiliana na changamoto hiyo.
Alisema kama
serikali imechukua hatua mbalimbali ambazo zitawezesha kukabiliana na tatizo
hilo la ajira kwa vijana hasa kwa kutumia mkakati wa Kilimo Kwanza ambapo baada
ya vijana kujinga katika vikundi watawezeshwa kupata zana za kisasa za kilimo
ili kumudu kulima kisasa na kuzalisha kwa tija na kupata kipato kwaajili ya
kupambana na umasikini.
Waziri
Wassira,alisema kuwa katika kuwezesha makundi maalum katika jamii yasiyo na
uwezo,tasaf awamu ya tatu itaanza kwa majaribio kwa wilaya za Bagamoyo,Kibaha
na Chamwino kabla ya mpango huo kusambazwa nchini kote.
Kuhusu ukame
ambao unaikabili wilaya hiyo,wasiri huyo alishauri viongozi kuanza kahamasisha
kilimo cha Mtama ambao umekuwa ukivumia ukame badala ya kuendelea na kilomo cha
za la mahindi.
Alisema
kilimo cha zao la mtama kiende sambasamba kilimo cha zao la alizeti ambapo
mbali na mtama kutumika kama chakula lakini zao la Alizeti linaweza kuwa zao
mbadala la biashara badala ya kung’ang’ania kilimo cha zao moja la pamba ambalo
limekuwa likiwaathiri wakulima bei inaposhuka katika soko la dunia.
Wakati huo
huo waziri Wassira,alisema serikali ya chama cha mapinduzi CCM,kuwa iko tayari
kutoa vibali vya ununuzi wa zao la pamba kwa mtu ama kwa taasisi yoyoyote ambayo itaweza kununua
zao hilo kwa bei ya juu ili kuondoa dhana kuwa serikali ndio inayohusika na
kushuka kwa bei ya zao hilo katika msimu huu.
Akizungumza
katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi Wassira,wakati akihutubia wananchi
wa kijiji hicho,alisema baada ya bei ya zao hilo kushuka katika soko la
dunia,kuna baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa
wakiwadanganya wananchi kuwa serikali ya ccm ndio inayohusika na kushuka kwa
bei ya zao la pamba wakati wakitambua wazi serikali haina uwezo huo.
Hata hivyo
amerudia wito wake wa kusema njia pekee ya kuondokana tatizo la kushuka kwa bei ya zao pamba kila
wakati,ni muda muafaka sasa wa kuweka wa
makusudi kwa wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba kuanza kutengeneza nyuzi
na nguo jambo ambalo pia litamkomboa
mkulima wa zao hilo.
No comments:
Post a Comment