Tuesday, September 25, 2012

Muda wa siasa ulikwisha mwaka 2010 sasa ni muda wa kuwahudumia wananchi bila ya itikadi-Airo         Mbunge wa Rorya Lameck Airo kushoto akiwa katika moja ya darasa  jimbo kwake
             Mawasiliano muhimu popote pale
 Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifurahi pamoja na watoto wa shule ya Msingi iliyopata msaada wa madawati

Rorya


MBUNGE wa jimbo la Rorya mkoani Mara Mh Lameck Airo,amewata ka viongozi hasa wa kisiasa kutambua kuwa uchaguzi tayari ulikwisha hivyo ni wawajibu wao katika kuwaletea maendeleo  wananchi wao bila ya kubaguana kwa misingi ya itikadi za kisiasa.


Mbunge huyo wa jimbo la Rorya,ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi,wananchi na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Obwere katika mji mdogo wa Shirati baada ya kukabidhi mdaa wa madawati kwa shule tatu za msingi za eneo hilo.


Amesema bado kuna viongozi wa kisiasa wameendelea kuwa na chuki na fitina kwa kushindwa kuwahudumia wananchi kutokana na msuguano ulitokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 jambo ambalo amesema halipaswi kupewa nafasi katika kuharakisha maendeleo ya wananchi Rorya.


Kwa sababu hiyo Mh Airo,amesema yeye kama mbunge amekuwa akipata vishawishi vingi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama chake cha CCM vya kumtaka kuacha kuhudimia vijiji na kata zinazoongozwa na wapinzani vishawishi ambavyo amesema hakubaliani navyo hata kidogo.


“Nimekuwa nikibanwa katika vikao vyetu vya chama kwamba kwanini napeleka maendeleo maeneo yenye viongozi wa upinzani lakini mimi nimepuuza kelele hizo kwani natambua wazi inawezekana sisi CCM tulifanya makosa kuwapelekea mgombea ambaye hawakumtaka sasa iweje leo tuwaadhibu”alisema na kuongeza.


“Umefika wakati tusahau tofauti zitu zote na kuacha itikadi za vyama vyetu katika kuwahudumia wananchi na tukifanya hivyo kwa kila kiongozi kwa mshikamano ninaamini Rorya itapata maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi tu”alisema Airo.


Kwa sababu hiyo amewataka viongozi wote katika jimbo hilo kuiga mfano wake na kuacha kuhudumia wananchi kwa misingi ya itikadi jambo ambalo linaweza kusababisha ubaguzi mkubwa ukiwemo wa koo na koo.


Mbunge Airo,alisema hivi sasa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo atahakikisha anapeleka katika shule zote za sekondari huduma ya maji safi na salama ili kuondolea adha wanafunzi ambao wamekuwa wakikatisha masomo kwa kufuata maji.


Naye diwani wa kata Mkoma Godwin Lazaro(Chadema)amempongeza mbunge huyo kwa jinsi anavyotumia kipato chake kwahudumia wananchi kwa kila sekta bila ya ubaguzi.


Alisema ingawa mbunge huyo anatokana na CCM lakini amekuwa na ushirikiano mkubwa na viongozi wote katika jimbo hilo jambo ambalo limefanya wilaya hiyo kuwa na mshikamano mkubwa ukiacha viongozi wachache wanashindwa kutambua mfumo wa kuwepo kwa vyama vingi nchini.


“Kwa niaba ya wananchi wa Mkoma,kwa kweli mbunge tunakuombea maisha marefu ingawa chama chako cha CCM tukikiombea maisha mafupi ila tunapaswa kuiga mfano mnzuri ambao wa mshikamano unatoonyesha sisi viongizi  na tukifanya hivyo kila mmoja nina uhakika hali ya leo ya maendeleo haiwezi kuwa sawa na kesho”alisema diwani huyo.


Hata hivyo diwani huyo wa Mkoma,alisema ni wajibu wananchi kuchangia maendeleo hasa ya sekta ya elimu katika maeneo yao na kwamba endapo hawataki kufanya hivyo wanapaswa kuacha kuzaa ikiwa ni njia moja wapo ya kuondokana na kero ya michango.


Kabla ya kupokea msaada wa madawati hayo,mwalimu mkuu wa shule ya Obwere Chiliko Magati,alisema shule hiyo pekee inakabiliwa na upungufu wa madawati 187 jambo ambalo limefanya idadi kubwa ya wananzi kusoma wakiwa wamekaa chini.


Mbali na shule ya Obwere kupewa msaada huo wa madawati shule nyingine ambazo zimenufaika na msaada huo ni pamoja na Kiariko na Ngasaro zote ziko katika eneo la Shirati.
kwa hisani ya www.georgemarato.blogspot.com

No comments:

Post a Comment