Monday, September 24, 2012

MH MKONO ANASTAHILI TUZO YA CWT BUTIAMA


         Walimu kujengewa Nyumba wakikubali kufundisha Butiama           

Elimu ni moja ya njia ambayo inaweza kumkomboa mwanadamu yeyote kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,kufanikisha kuwepo kwa elimu bora ambayo itapelekea mtu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine sharti suala la elimu lisimamiwe na mtu ili kufikia lengo huska

Pamoja na kufikia malengo huska lazima wawepo watu ambao watajitoa katika kufanikisha lengo hilo la kutengeneza mazingira ya Elimu kuwa bora,ili kufikia Malengo huska.


Mbunge wa jimbo la musoma vijijini Mheshimiwa Nimrod Mkono ni mmoja ya watu ambao wanatazamiwa kufikisha Malengo ya wakazi wa Jimbo hilo katika suala la Elimu kwa kujua kuwa elimu ndiyo ufunguo wa Maisha kwa nyakati za leo.

Kabla ya kuwepo kwake katika nafasi hiyo Jimbo la Musoma Vijijini pamoja na kupitiwa na wabunge mbalimbali,Mheshimiwa Mkono ameonekana kuwa shujaa katika Jimbo hilo hasa katika suala la kuboresha elimu katika jimbo hilo.Si wote wanaoweza kuthamini mchango wa huo maana waswahili wanasema unaweza ukashindwa kusoma lakini ukatazama picha.

Hivi karibuni Chama cha Walimu Tanzania katika wilaya ya Butiama mkoani Mara wamethamini mchango wa Mbunge huyo kwa kuangalia na kupima tangu kuwepo kwake madarakani kumekuwepo na Mafanikio Makubwa katika suala la elimu wilayani humo lakini pia amesaidia kutengeneza Mazingira rafiki ya Elimu katika eneo hilo.

Mchango huo unafuatia Shule nzuri zilizojengwa katika jimbo hilo ambapo kuna shule sita za Kimataifa huku Shule zaidi 40 akiwa ametoa mchango mkubwa katika kufanikisha Shule hizo kuwa Bora na Mazingira mazuri ya Wanafunzi kusoma na Walimu kufundisha.


KATIKA kukabilina na changamoto kubwa iliyopo katika Elimu hapa nchini Mbunge huyo alisema kuwa upungufu  wa walimu wa masomo ya sayansi unazozikabili shule nyingi hapa nchini ni Jukumu la Viongozi na Wanajamii kushirikiana kwa Pamoja kukabiliana nazo.

Katika kuonyesha dhamira ya dhati katika kupambana na suala la Elimu mbunge wa jimbo la Musoma vijijini mkoani Mara Nimrod Mkono ametangaza kumjengea nyumba ya kisasa kwa kila mwalimu wa somo la Sayansi  ambaye atakubali kufundisha somo hilo katika wilaya ya Butiama.

Katika ujumbe wa Chama cha Walimu Tanzania CWT katika wilaya ya Butiama hivi karibuni uliofika Kijijini kwake ukiwa na hati ya Pongezi na Tuzo ya Kinyago cha mfano wake wameonesha kutambua Mchango huo.Mbunge huyo wa Musoma vijijini  Mh Nimrod Mkono,alisema pamoja na kumjengea nyumba  kila mwalimu wa somo la sayansi pia atatoa fedha kwaajili ya chama cha kuweka na kukopa kwa kila shule yenye mchepuo wa masomo ya sayansi kuanzia sasa ikiwa ni njia ya kutengeneza Mazingira mazuri ya Elimu na kuwa kishawishi kwa watumishi wengi wa kada ya elimu katika Wilaya hiyo.

Akiongelea suala hilo Mbunge huyo alisema lengo la hatua hiyo ni kuvutia walimu zaidi kufanya kazi katika eneo hilo la butiama hasa kwa walimu wa sayansi na ambao ni wachache katika shule za Sekondari huku akiamini kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua suala la Elimu wilayani Butiama
 
Katika hafla hiyo ya Tuzo ya Kutambua huo Mbunge Mkono aliueleza ujembe huo wa cwt kuwa kulingana na mabadiliko ya makubwa ya dunia ya sayansi na teknolojia hakuna budi sasa kuongeza kasi katika ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za dunia.

“ Kutokana na Kasi ya Teknolojia natangaza  kuwa mwalimu yoyote ya soma la sayansi atakaekubali kuja kufundisha katika wilaya ya Butiama aje nimjengee nyumba nzuri na kisasa ili aweze kufanya kazi yake bila kupata tatizo la makazi”alisema Mkono na kuongeza.

                        Mh Mkono akipokea cheti kutoka CWT

“Mbali na nyumba pia nitatoa fedha za kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa kwa kila shule ya mchepuo wa sayansi katika wilaya yangu lengo langu likiwa nikuwavutia walimu zaidi kuja katika eneo hili na kufundisha bila vikwazo vyovyote”alisema.

Pamoja na nia nzuri ya Mh Mkono katika kuinua sekta ya Elimu katika jimbo la Musoma Vijijini ambapo kwasasa bado kuna changamoto kubwa kwa Walimu,Wanafunzi na Mazingira ya kufundishia ambapo hupelekea kila siku kuwepo kwa Migomo ya Walimu,Kuhusu migomo hiyo ambayo imekuwa ikijitokeza kila wakati  ya kushinikiza serikali kuboresha maslahi yao,mbunge huyo wa Musoma  vijijini amekishauri chama hicho kuanzia sasa kabla ya kufikia hatua ya kugoma kukutana nae hili kuona jinsi ya kutatua matatizo yao badala ya kugoma na kuwapa mateso  wanafunzi.


Katika kutambua Mchnago wa Walimu Mh Mkono alisema kuwa walimu wamekuwa na Matatizo Makubwa na kila siku kumekuwepo na Migomo na hivyo kusema kuwa huu sasa si wakati wa Mgomo katika Jimbo hilo.

Akitoa salama za CWT kabla ya kukatibidhi hati hiyo maalum na zawadi maalum kama ishara ya upendo na ushirikiano,katibu wa cwt wilaya ya butiama Wanjara Nyeoja,alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na mbunge huyo katika sekta ya elimu hasa kwa kujenga shule nzuri na za kisasa zikiwemo nyumba za walimu katika jimbo hilo.

Aidha alisema bado sekta ya elimu imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki zinazowakabili  shule za msingi na sekondari likiwemo tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za walimu.

“Walimu hususani maeneo mengi ya vijijini walimu wetu wanafundisha katika mazingira magumu kwa kukosa nyumba za kuishi hata kufikia walimu wengi kufikia hatua za kuhama wilaya yetu na kusababisha upungufu mkubwa wa walimu na wanaobaki sasa wazidiwa kazi ya kufundisha watoto wetu”alisema Nyeoja.

Hata hivyo katibu huyo wa  CWT,aliomba mbunge huyo kusaidia uanzishaji wa SACCOS ya walimu wa wilaya hiyo ambayo itasadia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia makali ya maisha yanawakabili walimu.

Kwa sababu hiyo,walimpongeza mbunge huyo kuonyesha mfano mkubwa wa kutumia raslimali zake kwaajili ya kujenga vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari zikiwemo nyumba za walimu katika jimbo hilo.

Kufikia Malengo ya elimu bora kwa kila Kijana wa Kitanzania sharti Makundi yote yaungane katika kuboresha elimu hiyo kama alivyojitolea Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijni Mheshimiwa Nimrod Mkono ndiyo maana nasema maboresho yaliyopo leo katika jimbo hilo “Tuzo hii alistahili”

No comments:

Post a Comment