Wednesday, September 26, 2012

MH BULAYA AENDELEA KUGAWA VIFAA VYA MICHEZO WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA

 Vifaa vilivyogawa kwaq kata 34 za wilaya ya Butiama mkoani Mara leo na Mh Esther Bulaya
 Mh Esther Bulaya akitoa neno kwa vijana wa kata 34 kutoka wilaya ya butiama mkoani Mara
 Katibu wa CCM wilaya ya Butiama mkoani Mara Bi Mercy Maramboakiwaasa Vijana wa CCM kutoka wilaya hiyo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama mkoani Mara Bw Gerald Joseph
 Picha ya Pamoja na Viongozi wa kata 34 za wilaya ya Butiama mkoani Mara wakiwa na nyuso za Furaha baada ya kukabidhiwa Vifaa hivyo
                               Baada ya shughuli niliweza kusalimia na Mh Bulaya

MUSOMA

Mbunge wa viti maalum kupitia vijana (CCM) Mh Ester Bulaya ameendelea kutekeleza  ahadi  yake ya kugawa vifaa vya michezo katika Jumuiya za Vijana wa Chama  hicho  Mkoani  Mara baada ya leo (jana)kugawa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 7.5 katika kata 34 kwa vijana wa Wilaya mpya ya Butiama mkoani hapa

Akikabidhi vifaa hivyo katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa,Bulaya alisema kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo katika michezo atahakikisha yale aliyoyakusudia katika  kutimiza azima yake kadri awezav katika kuhakikisha suala la Michezo linafanikiwa mkoani Mara
Alisema katika miaka ya nyuma Mkoa wa Mara umekuwa ukitoa wanamichezo wenye viwango vya juu katika michezo mbalimbali lakini katika kipindi cha hivi karibuni imeonekana kushuka kutokana na vijna wengi kushindwa kushiriki katika michezo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa vya michezo.

Mh Bulaya ambaye aliipatia  kila kata seti moja ya jezi pamoja na mpira alisema vijana wanaposhiriki katika michezo kuna faida mbalimbali ikiwemo kuibua vipaji pamoja na kujipatia ajira kupitia michezo na kuuomba uongozi wa vijana wa kata kuhakikisha timu zinakuwepo na kushiriki katika michezo ili vipaji viweze kuonekana na kuendelezwa.

Wilaya ya Butiama inakuwa Wilaya ya nne kupewa vifaa vya michezo baada ya kufanya hivyo katika Wilaya za Bunda,Serengeti na Musoma Mjini ,Mbunge huyo alisema kipaji chochote kitakachopatikana kupitia michezo ambayo itafanyika atahakikisha anampa sapoti katika vilabu vikubwa kama ambavyo amefanya kwa kipaji cha kijana aliyeibukia kupitia mashindano Ester Bulaya cup 2012 Wilayani bunda anayecheza katika timu ya yanga B.

Mbunge huyo alisema  kuwa ataendelea kusaidia michezo kadri atakavyoweza na pale anapopata nafasi na kudai kila kijana inampasa kushiriki katika michezo kwani licha ya kujipatia ajira pia anajijenga kiafya na kumfanya kushiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa kwa kuwa na afya bora.

akimkaribisha kuzungumza  na  vijana waliowakilisha katika kupokea vifaa hivyo,Katibu wa CCM Wilaya Butiama Mercy Marambo alisema Mbunge Bulaya ni mfano wa kuigwa katika Wabunge vijana kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana wenzake katika kuinua vipaji kupitia michezo.

Marambo alidai kupitia Ofisi yake ataendelea kutoa ushirikiano kwa Mbunge Ester Bulaya kwa kuwa ni Mbunge makini ambaye anafikra za kuhakikisha Vijana wenzake wanapata fursa mbalimbali zikiwemo za kushiriki katika michezo.. 

Pamoja na hivyo Mh  Bulaya alisema kuwa ingawa ataendelea kuchangia katika masuala ya Michezo mkoani Mara lakini pia Mbunge huyo aliendelea kuwahimiza Vijana kupambana ili kujikwamua katika suala zima la Kimaisha

No comments:

Post a Comment