Wednesday, September 26, 2012

MAONI YA MH NIMROD MKONO KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA HICHO.


Mmmoja ya watu walijitokeza kugombea uenyekiti kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi taifa Nimrod Mkono,amesema anaunga mkono kwa asilimia mia moja maamzi yote ya vikao vya uteuzi wa wagombea.

Alisema kuteuliwa yeye hakuna maana kuwa kuna jambo limekosewa bali ni taratibu za chama na kwamba kwa asilimia mia moja anaunga mkono uamuzi huo ambao umefanywa katika vikao mbalimbali vikiwemo vile vilivyokuwa chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete jana.“Mimi ni mwana ccm damu ninaunga mkono uamuzi wa chama changu tena kwa asimia mia moja,walioteuliwa ni wanaccm wenzangu ninatoa ahadi ya kuwapa ushirikiano wa kutosha hadi tutakapo pata mmoja wetu kuwa kiongozi wa jumuiya yetu”alisema Mkono.

Kuhusu kauli yake kuwa endapo hatapitishwa jina lake hapatatosha ndani ya CCM alisema kauli ile aliitoa kwa kusema kuwa hakubaliani nay ale yaliandikwa kwenye magazeti kwa vile kulikuwa bado kuna vikao vilikuwa vikiendelea ndani chama hicho.

“Nilisema sikubaliani nay ale yaliandikwa kwenye magazeti kwani wakati mchujo unafanyika sikuwepo hivyo huwezi kusema nilikuwa wamwisho wakati hata sikuwepo ndio maana nilisema sikubali kama kweli imekuwa hivyo kwa kuwa sikuwepo ila nilijua uamuzi ninaungoja ni wa vikao vingine na uamuzi umefanyika kwa haki na nimeridhika bila kingongo hivyo niwajibu wangu kukisaidia chama change”alisema

Aidha kuhusu kauli ya mwenyekiti wakewa taifa  watakashindwa kupitishwa watakihama chama hicho na kuwataka waende mapema,alisema hiyo ni kauli ya kiongozi wake ambayo yeye hajawahi kuitoa popote wala kutoa vitisho vya namna hiyo kwa chama chake.

No comments:

Post a Comment