Monday, September 17, 2012

MPWA WA GEORGE MARATO AKITIMIZA MOJA YA MILA ZA KIKURYA,PICHA 25 ZA TOHARA KATIKA KIJIJI CHA RYAMISANGA, PART 2

      *Picha  25 za sherehe ya Mpwa wake na  Mwandishi wa habari wa ITV & Redio one mkoani Mara George Marato,Mkazi wa kijiji cha Ryamisanga wilaya ya Butiama Mkoani Mara.Taarifa zinasema kuwa kwa mila ya Kabila ya Kikurya unapokaribia kutimiza Umri wa utu uzima lazima utairiwe na hivyo kuruhusiwa kuingia katika Mapenzi na kushiriki katika Tambiko zote za Kimila.

      *Lakini pamoja na kutimiza moja ya mila katika kabila hilo lakini pia wataalamu wa Afya wanasema kuwa mtu anapotairiwa ana zaidi ya asilimia 60 kujikinga na magonjwa Mbalimbali ukiwemo Ugonjwa wa Ukimwi,kufuatia hatua hiyo Serikali ya Tanzania iliamua kufanya zoezi hilo la kutairi baadhi ya Mikoa hapa Tanzania ukiwemo mkoa wa Mara katika wilya ya Rorya

   *   Matukio yote utayapata kupitia blog hii ya www.mwana wa Afrika.blogspot.com na
www.georgemarato.blogspot.com na  hapa ni Part 2

                            Jamaa wamekaa huku wakiimba nyimbo za kumpa kijana ujasiri kabla ya tohara
                      Mtaalam akiwa kazini na tayari kazi imeanza
  Tendo hilo kiukweli mwili ulisimka sana na hapo nami nilitupa jiko kujua nn kinaendelea
                  Mkurya mkurya tu,kijana hata kutikisika hakuna
   kama vile ndyo jamaa anaanza ebu cheki mtaalamu alivyoshika kisu
         Yaani dogo alivyosimama hata mguu haukusogea mbele
  Tayari jamaa kaisha punguza sehemu ya ngozi anavuta pumzi kutoa sehemu iliyosalia
   Sherehe ilianza Mwanzo baada ya kijana kukamilisha moja ya mila ya Kikurya kijasiri
 George Marato akiwa amebeba ngao ya kijana baada ya kuonuesha ushujaa katika tohara hiyo
    Safi sana aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

                              Mwita Waryoba akiwa tayari katimiza nguzo ya Kikurya
           Akina mama wakiserebuka baada ya kijana kuwa amefaulu hatua hiyo
  Huu ndyo usafiri uliotufikisha Ryamisanga na kurudi Manisapaa ya Musoma Salama,Tunamshukuru Mungu
    Mkurya mkurya tu hawezi kuacha asili,hapa George Marato akivalisha tayari kwa kuanza kucheza ngoma ya Kikurya
   Wanasema kazi na dawa,hata gari ikitaka kuondoka lazima uchek mafuta kama yatakufikisha katika safari yako,Marato akinywa Maji tayari kwa kuingia uwanjani kucheza ngoma ya LITUNGU

No comments:

Post a Comment